Alhamisi, 3 Desemba 2020

MADHARA YA PUNYETO

 

Tiba ya madhara ya upigaji punyeto.

Mwanaume mwenye mawazo

Kundi kubwa la wanaume wamepungukiwa uwezo wa tendo la ndoa kutokana na kitendo cha kupiga punyeto. Madhara haya ni pamoja na kuwahi kufika kileleni, kushindwa kurudia tendo na jogoo kuwa legelege. Makala yetu ya leo imeeleza kwa kina tatizo hili la kupiga punyeto na huduma ya dawa kwa wanaume wanaokwama kitandani. Endelea kusoma

Punyeto ni nini?

Punyeto ni tendo la mtu la kuamsha hisia za mapenzi au msisimko ambao unampelekea mtu huyu kufikia kilele cha kujimalizia tamaa zake! Bila kufanya tendo halisi, hutumia fikra zake katika picha za zinazoitwa za ngono au picha zozote zinazoweza kulifanikisha tendo hilo, movie n.k

Kilele cha yote anafikia mahali anajimalzia tamaa zake mwenyewe!. Nimekuwa nikiona baadhi ya watu wakipingana wao kwa wao katika suala zima la kupiga punyeto! Wako wanaotetea kutokana na elimu yao na wanasema kwa ujasiri mkubwa kwamba “kupiga punyeto ni sehemu ya maisha ya mwanadamu” Ina maana katika maisha ya mwanadamu upigaji punyeto inaelezwa ni kama tendo la lazima mpaka inafikia mahali wanasema ni sehemu ya maisha (Maisha) ya mwanadamu.

Ukubwa wa tatizo kwa vijana

Nimekuwa nikipata kesi nyingi sana juu ya madhara yatokanayo na punyeto. Aslimia 60 ya vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 30 wameathirika na tatzo hili na inakuwa ngumu kujinasua kutoka kwenye hili janga, kama wewe ni mmoja wapo na ulkuwa ukitafuta kwa mda mrefu ufanye nini ili uachane na tabia ya kupiga punyeto basi fatilia kwa makini makala hii

Madhara ya Upigaji Punyeto kwa Mwanaume

Haya ndio baadhi ya madhara ya kimwili ambayo yanaletekezwa na upigaji punyeto

1. PUNYETO INAUA NGUVU ZA KIUME:

Upigaji wa punyeto unaweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume, kwani kipindi unapiga punyeto jua ile mishipa inayofanya uume usimame unakuwa unaichua na uume unakuwa umesimama kwa muda mrefu sasa ikitokea ukawa unafanya hivi kila siku ile mishipa inalegea na uume unakuwa unakosa nguvu hata ukisimama haui strong unakuwa kama umelegea.

2. KUWAHI KUMALIZA MAPEMA KATIKA TENDO:

Mara nyingi mtu aliezoea kupiga punyeto huwahi kumaliza mapema pindi akiwa anafanya tendo la ndoa na wakati mwingine uume hushindwa kusimama kwa mara ya pili na kujikuta anashindwa kurudia tendo ikiwa mwenzake bado hajaridhika na anahitaji kuendelea kufanya tendo hilo.

Athari Nyingine za Kupiga Punyeto ni kama Zifuatazo

  • Uchovu wakati wote /
  • Maumivu ya nyonga na mgongo wa chini / Lower back pain.
  • Kusinyaa kwa Nywele na nywele kunyonyoka
  • Maumivu ya kende
  • Maumivu ya kiuno

Kuna faida nyingi sana ambazo utazipata endapo utaachana na tabia ya upigaji punyeto na hiyo napenda iwe sababu ya wewe msomaji kuachana hicho kitendo.
Kuacha punyeto ama mtindo flani wa maisha inahitaji utambuzi, uamue na pia uweze kjicontrol wewe mwenyewe, inahitaji nguvu ya ndani yako kushinda vishawishi , zifuatazo ni njia ambazo utaanza kutekeleza ukiwa nyumbani kwako bila gharama yoyote na zitaanza kukupa matunda, lazima uwe mwaminifu kufuata kile ninachoelekeza maaana ni njia ambayo imewasaidia vijana wengi.

1.PATA MDA MWINGI WA KUPUMZIKA

Baada ya shuguli za kawaida haikisha unapata mda wa kupumzika, lala mapema ili uweze kuipa akili mda wa kuchambua na kutunza taarifa za muhimu na kufuta zile zisizo za muhimu, angalau masaa 8 kwa siku. Hakikisha unalala mapema hapo ndipo utaongeza uwezo wa akili kuweza kupambana na hisia na mawazo mabaya.

2. MATUMIZI YA MBOGAMBOGA NA MATUNDA KWA WINGI

Utafiti wa kisayansi unaonesha kwamba matumizi mazuri ya vyakula vya mbogamboga na matunda Husaidia kuongeza uwezo binafsi wa kujisimamia juu ya tamaa na mihemko mbalimbali, matumizi ya vyakula vilivyosindikwa (junk foods) ni chanzo cha kushindwa kujizuia na hapo safari yako ya kuachana na upigaji punyeto itakwama.

3. FANYA MAZOEZI NA USHUGULISHE MWILI

Maozezi yanasaidia mwili kutofikiria kufanya mambo machafu sababu mara nyingi unakuwa bize, akili inapokuwa inashugulishwa basi uwezekano wa kuleta fikra mbaya ni mdogo sana

4. ACHA KUANGALIA PICHA ZA NGONO

Tafiti zinasema kwamba vijana wengi wenye umri kuanzia miaka 15 mpaka 30 ndo kundi kubwa lililoathirika kwa kutazama picha za pono, piacha au video za ngono huleta msukumo kwenye akili ili kuweza kujiridhisha na hivo hupelekea watu kupiga punyeto ili kukata ile kiu ya  tamaa zao za mwili. Anza leo kwa kufuta picha na video zote za ngono kwenye simu yako na ujiwekee mipaka kwamba hutazipakua tena.

NATURAL REMEDY PACKAGE KWA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.

Kifurushi cha kurejesha nguvu za kiume

Kwa kutambua kuwa vijana wengi wameathirika na tatizo la upigaji punyeto na wengine wakiwa wamekata tamaa  kwa kushindwa kuwaridhisha wapenzi wao kitandani basi tunakuletea  package ya siku 30 inayojumuisha dawa 2, zilizo katika mfumo Wa vidonge vilivyotengenezwa kiasili bila kemikali,  kwa bei ya punguzo sh 150,000/= tua mbayo itakusaidia kukurudisha katika hali ya kawaida karibu 80% hata kama ulishaathirika kwa upigaji punyeto.

Kifurushi chetu kina muunganiko wa dawa mbili za vig power na /codiceps. Dawa asili zilizofanyiwa utafiti na kuhifadhiwa katika mfumo wa vidonge  ambazo zitakusaidia

  • Kuongeza uzalishaji wa mbegu za kiume
  • Kuongeza ufanisi wa tendo la ndoa kwa kuimarisha kusimama kwa uume.
  • Kuongeza mzunguko wa damu kuelekea kwenye jogoo
  • Kuongeza hamu ya tendo la ndoa
  • Kusafisha figo
  • Kusaidia wenye matatizo ya jogoo kushindwa kusimama, na kushindwa kurudia tendo la ngono na
  • Kuweka mwili kuwa mchangamfu pasipo kuwa na maumivu ya viungo

UGUMBA

 

Soy Power Suluhisho la Ugumba kwa Wanawake

soy power

Je wafahamu kwamba Ugumba kwa mwanamke unatibika?Kama ukijua chanzo cha tatizo lako na ukatumia dawa sahihi tatizo lako litaisha na utaweza kushika ujauzito. Kwa bahati mbaya dawa nyingi zilizopo sokoni hazina ubora na hazilengi kutatua tatizo kiukamilifu. Najua unaweza kuwa umepoteza pesa nyingi kutibu shida yako ya ugumba bila mafanikio.

Soma makala yetu tuliyoandaa kuhusu ugumba kwa wanawake na sababu kwanini dawa kama Soy power imepata umaarufu sana katika nchi za wenzetu kutibu ugumba kwa wanawake kwa miaka mingi hata kuuzwa bei ghali hadi $66 sawa na 150,000 za kitanzania na ushuhuda wa wanawake waliowahi kutumia Soy power na kushika ujauzito ndani ya mwezi mmoja wa kutumia dawa.

Kama wewe ni mwanamke naamini bila shaka una ndoto ya kupata mtoto na kulea kwa siku za hapo mbele, vipi ndoto hii inapokatishwa na malengo yakabadilika kabisa.Takwimu za idadi ya wanawake wagumba zinaongezeka siku hadi siku duniani kote, huku lawama zikienda kwenye sumu zinazotuzunguka na lishe mbaya.

Ugumba Ni Nini?

Ugumba kwa mwanamke ni hali ya kutoweza kupata ujauzito kwa mwanamke pale ambapo unashiriki ngono pasipo kinga kwa muda wa mwaka mmoja. Kuna sababu nyingi zinazosababisha mwanamke kutoshika ujauzito, sababu hizi ni kama, Lishe mbaya, Msongo wa mawazo kupita kiasi, Athari ya Magonjwa ya zinaa, Matatizo kwenye tezi ya thairodi, Maambukizi ya fangasi ukeni, Kufanya mazoezi makali sana, Uzito mkubwa na kitambi na Mvurugiko wa homoni.

Mazingira Hatarishi na Sababu Zinazopelekea uwe Mgumba

Kikawaida mwanamke na mwanaume wanapokosa mtoto kwa muda mrefu huanza kufikiria kwamba tatizo lipo kwa mwanamke kitu ambacho maranyingi siyo kweli, mwanaume pia anaweza kuwa mgumba na mbegu zake kuwa dhaifu au kuwa chache na kushindwa kumpa mwanamke mimba. Nashauri pale mnapogundua kuna shida kama hii basi wote wawili nendeni hospitali mkapime kujua nini chanzo cha ugumba.

Mazingira mengi hatarishi ambayo hupelekea mwanamke kuwa mgumba unaweza kabisa kuyaepuka, mazingira haya ni kama lishe mbaya, msongo wa mawazo, uvutaji wa sigara na kunywa pombe, uzito mkubwa na kitambi, matatizo ya tezi ya Thairodi na magonjwa ya zinaa. Sababu pekee ambayo ni vigumu kuepuka ni umri, kadiri umri unavoenda ndivo uwezo wa kushika mimba unapungua. Mazingira haya hatarishi hupelekea matatizo kwenye uzazi kama

  • Mayai kutopevuka
  • Ugonjwa wa vimbe kwenye mifuko ya mayai Polycystic ovarian syndrome
  • Kiwango kikubwa cha homorne ya prolactin ambacho huhusika na utengenezwaji wa maziwa ya mtoto.
  • Majeraha kwenye mirija ya uzazi ama kuziba kwa mirija ya uzazi na
  • Kukua kupita kiasi kwa tishu za mfuko wa mimba (endometriosis)

Nitajuaje Kama Mimi ni Mgumba

Kwa kutazama dalili hizi hapa chini unaweza kujifahamu kama wewe ni mgumba

  • Kushindwa kushika ujauzito kwa zaidi ya miezi 6 mpaka mwaka
  • Kuwa na mzunguko mrefu wa hedhi zaidi ys siku 35 ama chini ya siku 21
  • Hedhi kuvurugika na kubadilika badilika
  • Kukosa hedhi kabisa; hii inaweza kuwa kiashiria na mayai kutopevuka

Habari njema ni kwamba wanawake wengi wameshika ujauzito baada ya kutumia kirutubisho cha Soy power kupevusha mayai. Ngoja nikupe maelezo jinsi gani Soy power itarudisha matumaini yako na ukapata ujauzito mapema ili uwe shuhuda wetu kwa wagonjwa wengine.

 SOY POWER

 SOY POWER NI KITU GANI HATA KIWE ADIMU ZAIDI?

Soy power ni kirutubisho kilichotengenezwa nchini Marekani baada ya kufanyiwa utafiti wa kisayansi kwenye maabara kwa muunganiko wa mimea tiba aina tano ambayo ni Semen Glycine, Radix Paeoniae Alba Extractum, Ganoderma, Soy Isoflavones. Kirutubisho hiki kimekuwa maarufu sana kwenye nchi za wenzetu kama Marekani, China na India kwa kutibu ugumba kwa wanawake na kuzuia saratani ya matiti.

Kazi na Faida za Soy power kwa Mwanamke

  1. Kuimarisha utendaji wa ovari na mayai kupevuka kwa wakati
  2. Kurekebisha homoni za kike na hivo kuimarisha uwezo wa kushika mimba
  3. Kuzuia saratani ya matiti
  4. Kupunguza kasi ya uzee, kungarisha afya ya ngozi
  5. Kupunguza upotevu wa uimara mifupa hasa kwa wanawake waliokoma hedhi.

SOY POWER INAWAFAA ZAIDI

  • Wanawake waliokosa mimba kwa mda mrefu
  • Wanawake wenye mvurugiko wa homoni
  • Wanawake wenye mtatizo ya hedhi
  • Wanawake wenye ugumba kutokana na kiwango kidogo cha estrogen
  • Wanawake ambao wamekaribia ama wameshakoma hedhi na
  • Wanawake wanaokosa hamu ya tendo la ndoa na kukosa usingizi mzuri.

Kisimi kinawasha

 

Kwanini Kisimi kinawasha na Kuvimba?

Utangulizi kuhusu Kisimi

Kisimi au kinembe ni kiungo kinachoonekana mwanzoni mwa uke kwa juu, kazi ya kiungo hiki ni kuchochea hisia na kumfanywa mwanamke kufikia kilele katika tendo la ndoa. Kisimi kinaweza kuonekana kidogo kwa juu lakini napenda ufahau kwamba kisimi kimejichimbia zaidi kueekea ndani kama mzizi na ni kiungo kikubwa. Tutazungumzia changamoto kadhaa wanazopata wanawake kama kisimi kuvimba, kupanuka, na kuwasha. Endelea kusoma kufahamu zaidi.

Je kuna Size Sahihi ya Kisimi?

Japo hakuna kiwango cha kawaida cha kisimi, lakini najua wafahamu kiwango au size ya kila siku ya kisimi chako. Mara kadhaa kuna baadhi ya hali au shughuli huweza kusababisha kuvimba kwa kisimi kwa muda flani mfano kuongezeka kwa hisia za mapenzi, na kuna sababu zinazoweza kupelekea kuvimba kwa kisimi kwa muda mrefu.

Kuvimba kisimi kwa siku chache

Kuvimba kisimi kwa mda mfupi ni kawaida kama mwanamke ameamshwa kihisia. Hisia za kimapenzi zinapokuwa juu,mzunguko wa damu huongezeka kuelekea kwenye via vya uzazi. Kisimi pamoja na mashavu ya uke huongezeka ukubwa katika hichi kipindi, na kupungua ukishafika kileleni.
Kama mwili wako unasisimuliwa mara kwa mara kimapenzi, na usifike kileleni, basi kisimi kinaweza kuendelea kuwa kimetutumka kwa mda mrefu zaidi.
Vitu vimngine ikiwemo maambukizi vinaweza kuwa chanzo cha kuvimba kwa kisimi pamoja na mashavu ya uke. Mashavu ya uke yanaweza kuvimba kutokana na
Aleji na vifaa au kemikali, nguo, cream au manukato
Maambukizi ya fangasi na bacteria
Kupiga punyeto na kuingiliwa na kitu kwa muda mrefu kwenye uke.

Kuvimba kisimi kwa Zaidi ya wiki

Kama tatizo linafikia wiki moja na zaidi linaweza kuwa limesababishwa na

Matatizo ya homoni

Kuwa na homoni nyingi za kiume (androgens) kama testosterone huweza kupelekea kisimi kuongezeka ukubwa.

  • Wanawake wenye polycystic ovarian syndrome (PCOS) na matatizo mengine ya homoni wanapata changamoto hii ya kukua kwa kisimi.
  • Vimbe kwenye Mayai (Ovarian Tumors)
  • Uvimbe kwenye mifuko ya mayai huanza kuzalisha homoni za kiume kwa wingi na hivo kuepelekea kuongezeka kwa ukubwa wa kisimi.

Lini unatakiwa Kumwona Daktari

kama kisimi au kinembe chako hakirudi katika hali ya kawaida ndani ya siku mja basi unatakiwa kumwona daktari. Unatakiwa pia kumwona daktari kama unapata dalili zingimne kama maumivu na kutokwa na majimaji aidha damu au uchafu. Ni kwa sababu dalili hizi zinaweza kuashiria maambukizi kwenye uke.Hakikisha unamwona daktari unapoona tu dalili zisizo za kawaida. Usisubiri mpaka tatizo liwe kubwa.

HEZI SARAMA

 

Mwongozo wa hedhi salama

Hedhi salama ni ipi

Kwa mwanamke kuwa na mzunguko mzuri wa hedhi ni jambo la kujivunia na linaloleta heshima kwako kama mwanamke.
Mzunguko wa hedhi unaweza kutoa picha kamili nini kinaendelea kwenye mwili wa mwanamke, kama mfuko wa mimba unapata mzunguko mzuri wa damu, homoni zako zinbalansi, au kama mayai yanatolewa kwenye ovari. Katika makala yetu ya leo tutaangali hatua za mzunguko wa hedhi, jinsi ya kutumia viashiria ya hedhi ili kujua afya yako na jinsi ya kutumia tiba asili (natural therapies) kama fertility cleansing, tiba za mimea, ama lishe katika kuweka mzunguko wenye afya.

Hedhi ni kitu gani?

Hedhi ni muunganiko wa yai ambalo halikurutubishwa pamoja na damu inayotokana na kumomonyoka kwa tishu laini za ukuta wa mfuko wa mimba (uterus). kitendo hiki hutokea kila mwezi kwa mwanamke.
Jinsi mwili unafofanya kazi mpaka kupatikana kwa hedhi
Kupata hedhi ni kitendo kinachoratibiwa na mzunguko wa homoni . Kwa maelezo mafupi na rahisi ni kwamba inaanza na eneo la ubongo linaloitwa hypothalamus kuzalisha homoni ya gonatrophin (GnRH) ambazo zinachochea tezi ya pituitary kuzalisha homoni ya luteinizing(LH) na Follicle stimulating hormone(FSH), homoni hizi mbili yaani LH na FSH hulenga kuamrisha Ovari kuzalisha homoni za estrogen na progesterone. Ovari napenda kuita ni kiwanda cha kuzalisha na kuhifadhi mayai.
Kwa haraka unaweza kusema ni kitendo rahisi, fikiria hmomoni hizi zinafanya kazi kama vile mfano wa vitabu vilivyopangwa mezani kwa wima vikilaliana, ikitokea kitabu cha mwanzo kimeondolewa kwenye mstari basi vyote vinaanguka.Nii mlolongo mrefu na kama ikitokea mvurugiko wa homoni moja basi mtiririko wote unaharbika na unaanza kukosa hedhi au hedhi kuvurugika, na matatizo mengine mengi ya uzazi ikiwemo uvimbe na ugumba. Zifuatazo ni hatua za mzunguko wa hedhi.

Hatua za Mzunguko wa hedhi

  1. Follicular phase

    Sehemu ya ubongo inayoitwa hypothalamus hutambua kiwango cha estrogen na progesterone ambacho huzalishwa na ovari. Kama kichocheo cha estrogen kikipungua ndani ya mzunguko wa hedhi basi ubongo hutoa GnRH ambayo huamrisha pituitari kuzalisha FSH ambayo inachochea kuanza kukua kwa mayai kuanzia 10 mpaka 20, kati ya haya ni yai moja pekee ambalo hukomaa na kuwa tayari kurutubishwa ndani ya mwezi husika.
    kadiri mayai madogo yanavokuwa huzalisha homoni ye estrogen ambayo kazi yake ni kuimarisha na kuundaa ukuta wa uterus ili kupokea kiumbe baada ya urutubishaji kufanyika.
    Kadiri kiwango cha estrogen kinavyopanda ndivyo mwanamke ataanza kupata ute mzito wa rangi ya maziwa. KUongezeka kwa kiwango cha estrogen huchochea utolewaji wa GnRH kutoka kwenye ubongo ambayo huchochea FSH na LH kwa wingi, homoni hizi mbili huchangia utolewaji wa yai kwenye kikonyo chake kitendo hiki huitwa ovulation. Baada ya ovulationlation kiwango cha FS na LH huanza kupungua taratibu.

  2. Luteal phase
    Kutolewa kwa yai unafuatiwa na hatua hii ya Luteal. kabla ya kuendelea nataka ufahamu baadhi ya misamiati: Kumbuka baada ya yai kutolewa kwenye kikonyo linabaki kovu kama shimo, kovu hili huitwa corpus luteum, kazi yake ni kuendelea kuzalisha progesterone na kiwango kdigo cha estrogen. Ukuta wa juu mwembamba wa uterus ambao humomonyoka tunauita endometrium. Kwahivo baada ya yai kutolewa progesterone inasaidia kuendelea kuurutubisha ukuta(endometrium) ili uweze kupokea kiumbe.
    Endapo hapatawepo na mbegu ya kiume(sperm) kurutubisha yai basi ukuta wa endometrium huanza kubomoka na kutolewa nje kama hedhi.

Jinsi ya Kuhesabu Siku za Mzunguko wa Hedhi

Siku ya kwanza ya mzunguko ni siku ambayo unapata hedhi katika mwezi husika. Siku zote kati kuanzia siku ya kwanza ya hedhi mpaka siku ya ovulation (yai kutolewa) huitwa follicular phase. Kipindi hiki kikawaida huchukua siku 14 lakini hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke.
Luteal phase ni kipindi kati ya ovulation(siku ambapo yai limetolewa) na siku ya kwanza kupata hedhi katika mwezi,ni katika kipindi hiki ambapo yai lililorutubishwa hujishikiza kwenye ukuta wa uterus. Kama kipindi (luteal phase) kitakuwa kifupi sana chini ya siku 12 basi itakuwa ngumu kwa kiumbe kujishikiza kwenye ukuta.

Hedhi ya Kawaida ni ipi

Najua wanawake wengi mtakuwa mnajiuliza ni mzunguko gani wa hedhi ambao ni wa kawaida kwa mwanamke kuwa nao. Ukweli ni kwamba hakuna jibu la mojakwamoja kwamba mzunguko ule ni wa kawaida kutokana na kwamba miili imetofautiana. Lakni taarifa muhimu za kujua kama mzunguko wako ni mzuri ni kujua jumla ya siku za mzunguko wako, kiwango cha maumivu wakati wa hedhi, rangi na kiwango cha bleed yako, taarifa hizi zinaweza kukusaidia kujua ni aina gani ya lishe au tiba asilia utumie ili kurekebisha na kubalansi hedhi yako.

Urefu wa Mzunguko wa Hedhi

Mzunguko wa kawaida unatakiwa kuchukua siku 21 mpaka 35. Baadhi ya wanawake wanaweza kuwa na mzunguko mfupi zaidi au mrefu kuliko huu. Kiwango cha homoni na utolewaji wa yai ndivyo vinatengeneza uwiano wa mzunguko wa hedhi. kama yai halitatolewa itapelekea kuvurugika kwa hedhi na tena kupelekea yai kutotolewa, inakuwa ni kitu endelevu. Kuna vihatarishi vingi vinavyoweza kuvuruga homoni za kike kimojawapo ikiwa ni msongo wa mawazo.

Jinsi ya kutumia Viashiria vya Hedhi ili Kutambua Uwiano wa Homoni Zako.

Hapa chini nimeelezea uhusiano kati ya viashiria hivi na homoni zako. Lengo langu ni kukuonesha namna ya kuusoma mwili na kuusikiliza pale unapoeda nje ya mstari. Mzunguko wa hedhi ni njia muhimu ya kuusoma mwili kuhusu uwezo wa kushika mimba.

  • Kukosa hedhi
    Kukosa hedhi mara moja inaweza isiwe tatizo. Mpangilio wa homoni ni kitu sinsitive sana na kinaweza kuathiriwa tu na msongo wa mawazo, lakini kwa kiasi kikubwa unaweza kujirekebisha wenyewe. Kukosa hedhi pekee siyo kiashiria kwamba hutaweza kushika mimba, manake yawezekana mayai yanatolewa(ovulation) lakini usipate hedhi. Kukosa hedhi kwa zaidi ya miezi 6 huitwa Amenorrhea na inaashiria kuna tatizo ambalo unahitaji kumwona Dactari haraka.
  • Period fupi
    Mzunguko mfupi unaweza kuleta matatizo kwenye uwezo wa kushika mimba. Baadhi ya vihatarishi ambavyo hufupisha mzunguko wako ni kama kukosa ovulation, upungufu wa virutubisho mwilini, uzito mdogo sana, upungufu wa damu .
  • Period ndefu
    Mzunguko mrefu wa hedhi unaweza kuashiria kuvurugika kwa homoni na yai kutotolewa kwa yai kwenye kikonyo chake. Homoni ya progesterone ambayo hutolewa na mwili husaidia kuzuia bleed kuemdelea. Kama estrogen ni nyingi na progesterone ni kidogo bleed inaweza kuendelea kwa siku nyingi zaidi kuliko kawaida
  • Hedhi nzito na nyingi zaidi
    Kupata hedhi nzito na nyingi kupita kiasi husababishwa na ukuta wa uterus kusisimka zaidi kutokana na wingi wa estrogen, inapelekea ukuta kumomonyoka kupita kiasi. Tatizo hili linaweza kurekebishwa kwa kurekebisha lishe yako na kutumia tiba ya mimea kwa ajili ya kurekebisha homoni. Upungufu wa vitamin A na C inaelezwa kuchangia bleed nzito. unaweza kutumia Virutubisho kama Multivitamin.
  • Hedhi kidogo inayoambatana na maumivu makali ya tumbo
    Kama unapata hedhi nyepesi, nyekundu inaweza kuashiria kwamba mzunguko kwenye mfuko wa mimba ni mdogo. Unaweza kupunguza hali hii kwa kufanya masaji kwenye eneo la tumbo ukitumia mafuta ya castor,ama kitambaa kilicholowekwa kwenye maji ya moto.
  • Hedhi ya damu nyekundu inayong’aa
    Kama hedhi yako inakuwa ni damu nyekundu inayong’aa basi hakuna tatizo endelea kufurahia hedhi yako.
  • Hedhi nzito yenye weusi ama brown
    Hii inaonesha kwamba kuna masalia ya damu ya zamani kwa hedhi iliyopita. Kubaki kwa damu husababishwa na flow ya polepole sana na mzunguko mdogo ndani ya mfuko wa mimba. Unaweza kurekebisha tatizo hili kwa kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha, kufanya masaji eneo la tumbo na pia unaweza kujaribu fertility cleansing package yetu.
  • Hedhi yenye damu mpauko na maji zaidi.
    Kama unapata hedhi ya namna hii inaonesha kwamba damu yako kiujumla haina ubora na inakosa virutubishi muhimu. Kula lishe nzuri husaidia unaweza pia kutumia virutubishi vingine kama Multivitamin na Spiriluna kuimarisha damu yako.
  • Kuganda kwa damu ya hedhi
    Kuganda kwa damu ya hedhi inaweza kuwa siyo jambo na kutisha ukilinganisha na kuganda kwa damu kwenye mishipa ya damu. Lakini yatakiwa kuendelea kufatitilia hedhi yako pia. Kama kuganda kwa hedhi yako kunatokea mara chache hasa mwanzoni mwa period, ni mabonge madogo madogo, yenye rangi nyekundu inayong’aa basi ni salama. Lakini kama unapata mabonge mabubwa na inakuwa mfululizo basi yahitaji kumwona Dactari kupata ushauri. Unatakiwa kumwona Dactari haraka kwani kupata Damu nzito yenye mabongemabonge kama unahisi unaweza kuwa na ujauzito yaweza kuashiria kwamba mimba imeharbika.Tumia maji ya kutosha na kufanya masaji eneo la tumbo kwa kutumia mafuta ya nyonyo (castor) ili kupunguza tatizo hili.
  • Kupata bleed kwenye kipindi kisichokuwa na hedhi
    Bleed katikati ya vipindi vya hedhi ni tatizo linasowachanganya sana wanawake. Yaweza kusababishwa na kuvurugika kwa mpangilio wa homoni (rejea maelezo yangu pale juu)Yai kutotolewa kwenye kikonyo chake(ovulation),
    Uvimbe unaotokana na kukua kupita kiasi kwa tishu laini za ukuta wa uterus(endometriosis),Matumizi ya dawa za kupanga uzazi, Mazoezi magumu naLishe duni
  • Kukosa kabisa hedhi(Amenorrhea)
    Inaweza kutatiza pale ambapo unashika ujauzito lakini hupati hedhi kabisa. Kuwa na mzunguko mzuri ni hatua ya kwanza katika kujua kwamba unaweza kushika ujauzito. Kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kuchangia hedhi yako kuvurugika kama msongo wa mawazo, lishe duni, uzito mdogo sana, kutumia vidonge vya kuzuia mimba, kuvurugika kwa homoni, umri kwenda (kukaribia menopause) na matatizo mengine ya kiafya.

Hatua 4 za kufuata ili kuhakikisha kwamba unapata mzunguko mzuri wa hedhi.

  1. Kusawazisha vichocheo/hormones

    Kama nilivokwisha kueleza pale juu kuna mstari mwembamba sana kati ya hedhi kuwa sawa na kuvuruga kwa hedhi, makosa kidogo tu yanaweza kupelekea kuharibu mpangilio wa vichocheo na hivo kuvuruga hedhi yako. Tumia virutubisho mbalimbali kama Soy power, chai ya Pine pollen na Multivitamin kweka sawa vichocheo vyako.

  2. Kuimarisha uwezo wa ini.
    Ini pamoja na kazi zingine hufanya kazi ya kuondoa homoni zilizozidi mwilini. kama kuna kiwango kikubwa cha estrogen ini linaweza kuzidiwa na kuhitaji usaidizi. Hakikisha unatumia tiba nzuri za mimea na virutubishi asili kusafisha ini lako kila mwezi.
  3. Lishe
    Lishe inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuweka hedhi yako sawa. Ni muhimu kutumia virutubisho vya aina nyingi ikiwemo vitamins, madini, mafuta, vidondoa sumu(antioxidants). Vyakula hivi ni muhimu kutumia kwa wingi kwenye mlo wako wa kila siku. Hakikisha unapangilia ili kila siku upate virutubisho hivi vyote kwenye milo yako.Hapa chni nimeelezea vyakula kwa kila aina vya virutubishi . Nimekupa uhuru wa kupangalia kila mlo, siyo lazima kula vyakula hivi vyote kwa mara moja,lakini ni uhimu kupata virutubisho vyote kwa siku. Vyakula vingi vina vitamin na madini mengi uataona maelezo hapa chini.

     

    • madini ya chuma: vyanzo ni mboga za kijani, maini, mayai na mbegu za maboga(unaweza kutumia pia unga wake kutengeneza chai, ama kuchanganya na uji)
    • Vitamin C na B: vyanzo hoho nyekundu, machnungwa, broccoli, cabbage, nyanya na cauliflower.
    • Omega 3: vyanzo vyake samaki, walnuts, na chia seeds
    • Fibers au kambakamba : vyanzo ni mboga za majani kwa wingi na vyakula visivyokobolewa.
    • Madini ya zinc: mbegu za maboga na nyama
    • Vitamin D: kwa kupata mwanga wa jua walau dak 15 mpaka 20 kila siku. asubuhi au jioni
    • Vitamin E: vyanzo vyake ni mafuta ya olive, spinach, parachichi na almonds
    • Folic acid: vyanzo vyake: maini, spinach na maharage.
    • Vyakula vyenye mafuta mazuri; vyanzo ni mafuta ya nazi, olive, parachichi na karanga
  4. Punguza Msongo wa Mawazo
    Stress huleta matoeko hasikwenye hedhi yako kama usipoweza kujifunza namna ya kudhibiti. Stress za kazi, familia, uchumi binafsi na mengine mengi huvuruga mpangilio wa homoni zako. Stress huongeza utolewaji ya homoni ya cortisol ambayo huzuia uzalishaji wa GnRH (rejea maelezo yake pale juu) na kisha kupelekea mayai kutotolewa kwenye kikonyo(ovulation). Stress kwa wanaume hupunguza uzalishaji wa mbegu za kiume na hamu ya tendo la ndoa kwa wote. Mazoezi husaidia kupunguza athari ya msongo wa mawazo.

Muhimu Kwa mwanamke mwenye Changamoto ya Hedhi

Kwa mwanamke mwenye changamoto ya hedhi kuvurugika ama kukosa hedhi kwa muda mrefu, tunashauri atumie mafuta haya ya Rose , yanasaidia kurekebisha homoni. Mafuta haya yalitotengenezwa kitaalamu kwa kuzingatia uasili wake kutatua changamoto za wanawake kama kukosa hedhi, maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi na kukosa hamu ya tendo

rose oil
mafuta ya rose

Angalizo wakati Unatumia Mafuta ya Rose

Kuna tofauti kati ya mafuta ya rose,rose water, mafuta ya rosemary na mafuta ya primrose. Mafuta mengi ya rose yaliyopo mtaani hayana ubora unaotakiwa na ndio maana tumejitahidi kufanya utafiti na kukuletea mafuta yetu asili ya Rose yasiyochakachukuliwa kwa kuendana na thamani ya pesa yako ili

MIMBA YA MAPACHA

 


Jinsi ya kupata Mimba Mapacha

mapacha wanaofanana

Mimba ya Mapacha

Kwa miaka ya hivi karibuni wanawake wamekuwa wakichelewa sanaa kuanza familia ukilinganisha na miaka ya zamani,ambapo wanawake walikuwa wanaolewa wadogo mpaka miaka 15 wanaanza kujifungua.

Kutokana na hili wanawake kuzaa mapacha imekuwa zaidi kuliko zamani, kwasababu chansi ya kuzaa mapacha ni kubwa kwa wanawake wa umri zaidi ya miaka 35 na waliopata ujauzito kwa kutumia dawa zaidi(fertiliy treatment).
kama nawe unataka kuzaa mapacha fahamu kwamba hakuna formula moja kamili ya kufuata lakini kuna baadhi ya njia unaweza kurekebisha ili kuongeza chansi ya kushika mimba ya mapacha. Fuatana nami na mwisho wa makala utaweza kuamua kama ujaribu bahati yako au la…

Mimba ya Mapacha hupatikanaje?

Mimba hutungwa pale mbegu ya kiume inapokutana na yai la mwanamke na kulirutubisha. Kama kwa kipndi ambacho mke na mume wamekutana kuna mayai mawili yametolewa au yai moja liliorutubishwa kugawanyika kuwa mawili basi mwanamke hupata mimba ya mapacha.

Ainza za Mapacha

Mapacha wanaofanana (identical twins): aina hii ya mapacha hufanyika endapo yai moja liliorutubishwa kugawanyika vipande viwili. Mapacha hawa hufanana vinasaba, sura na jinsia pia.

Mapacha wasiofanana(fratenal twins): Aina hii ya mapacha hutokea pakiwa na mayai mawili yaliyokomaa kwenye kizazi wakati wa urutubishaji, na mbegu za kiume kurutubisha mayai yote mawili. Mapacha hawa wanakuwa na jinsia na vinasaba tofauti.

Kwanini mwanamke anajifungua mapacha, nini hutokea?

Mpaka sasa hakuna sababu za moja kwa moja kuonesha ni jinsi gani mpaka mapacha wanafanyika. Japo baadhi ya sababu huweza kuongeza chansi ya kupata mapacha, sababu hizi ni kama

Umri wa Mwanamke

Tafiti zinasema kwamba wanawake wenye umri mkubwa hasa kuanzia miaka 35 wana chansi kubwa ya kupata mapacha wasiofanana. Hii ni kwa sababu ovari za mwanamke huanza kutoa yai zaidi ya moja kila mwezi katika umri huo. sababu ingine ni kwamba wanawake wa umri mkubwa hutoa kichocheo cha FSH(follicle stilumating hormone kwa wingi) ambacho kazi yake ni kuchochea upevushaji wa mayai.

Familia kuwa na Historia ya Kuzaa Mapacha

Kama kwenye familia yako kama mwanamke ama kwenye familia ya mwanaume kuna mapacha basi una uwezekano mkubwa wa kupata mimba ya mapacha pia.

Kuwa kwenye tiba za kuongeza upevushaji wa mayai

Tiba za changamoto za uzazi ni njia maarufu sana kwatika kushika mimba ya mapacha. Vidonge vya tiba hizi huchochea uzalishaji wa mbegu za kiume na mayai ya mwanamke. Kama mayai mengi yakizalishwa kuna uwezekano kwamba yai zaidi ya moja litakuwa tayari kwa urutubishaji kuongezeka na hivo mimba ya mapacha kupatikana.

IVF(invitro fertilization)

IVF ni njia ya maabara ambapo daktari anatoa yai kwenye kizazi na kisha kupandikiza mbegu ya kiume nje ya kizazi kisha kiumbe kupandikizwa kwenye kizazi tena ili kukua. Njia hii ni ghali na wachache huweza kumudu Gharama zake zaweza kufikia sh milioni 24 za kitanzania.

Muhimu pale unapojaribu bahati yako kupata mapacha kupitia huduma yetu.

  • Pumzika kwa muda mrefu kati ya mimba moja na nyingine. Hii itasaidia mayai kutengenezwa kwa wingi na hivo kuongeza uwezekano wa kupata mapacha.
  • Wenza wote mke na mume wanatakiwa kutumia virutibisho, hivyo ni vyema kushirikishana katika hili ili muweze kushirikiana kufanikisha zoezi.
  • Huduma hii siyo ya uhakika kwa 100% hapana, ni jambo la kuongeza uwezekano , kadiri unavozingatia maelekezo yetu na kutumia virutubisho ndivyo unaongeza uwezekeno wa kupata mapacha
  • Kama una changamoto za uzazi inabidi tukupatie tiba kwanza kabla hujaanza hili zoezi.
  • Zoezi hili litawafaa zaidi wanawake wa umri kuanzia miaka 35 na kuendelea

KIZAZI KUINAMA

 

kizazi kuinama (retroveted uterus)

Kizazi kuinama.

Je umewahi kusikia kuhusu kizazi kuinama?, pengine ndugu , rafiki ama mke wako amefanyiwa vipimo na kugundulika kwamba kizazi chaje kimeinama. Leo nitakupa tafsiri nzuri ya kuinama kwa kizazi na jinsi gani inavoathiri afya ya uzazi kwa mwanamke.

Kuinama kwa kizazi kwa majina mengine ya kitaalamu tunaweza kuita tilted uterus,retroflexed uterus, retroveted uterus au backward uterus ni namna mfuko wa mimba unapovutika kuelekea nyuma zaidi ya mlango wa kizazi badala ya kuvutika kuelekea mbele. Ili uweze kunielewa vizuri angalia picha hapa chini. Picha ya kushoto inaonesha kizazi (uterus) cha kawaida na kinaonekana kimepinda kuelekea upande wa mlango wa kizazi. Picha ya kulia ndio inaonesha kizazi kuinama kuelekea nyuma zaidi.

kuinama kwa kizazi

Dalili Anazopata Mwanamke Mwenye Kizazi Kilichoinama

Kumbuka siyo lazima kupata dalili zote kwa pamoja, kama unapata dalili zisizo za kawaida ni vizuri kufika hospitali ili kufanya vipimo ukaanza tiba mapema. Sasa baada ya kuona dalili tuangalie uhusiano kati ya kizazi kuinama na afya ya uzazi.

Nini Kinasababisha Kizazi kuinama?

Mfuko wa mimba ambacho ndio kizazi tunachozungumzia ni sehemu tupu ambayo inajiweka katika eneo la chini ya nyonga za mwanamke. Kazi yake ni kuhifadhi kichanga baada ya urutubishaji kufanyika. Kizazi cha mwanamke kinaweza kuinama kutokana na sababu mbalimbali kama

  • Kulegea kwa misuli ya nyonga: mwanamke akishafikia kukoma hedhi au baada ya kujifungua, misuli inayosapoti tumbo la uzazi hulegea na hivo kupelekea kizazi kuanguka kwa nyuma kama picha pale juu inavooensha.
  • Kupanuka kwa kizazi kutokana na ujauzito, ama vimbe mbalimbali kama fibroids au vimbe ambazo ni saratani (tumor) zinaweza kusababisha kuinama kwa kizazi.
  • Makovu ama msuguano kwenye nyonga
    Mfuko wa mimba ama kizazi kinaweza kupata makovu kutokana na hali mbalimbali mfano , maambukizi kama PID, uvimbe(endometriosis) ama makovu kutokana na upasuaji uliowahi kufanyiwa kwa kipindi cha nyuma. Makovu haya yanaweza kufanya kizazi kuvutika kuelekea nyuma na kuinama.

Kizazi Kuinama na Uwezo wa Kushika Ujauzito.

Kuinama kwa kizazi inaweza kupelekea ugumu wa kushika ujauzito Lakini athari hii siyo ya mojakwamoja, madaktari wanatakiwa kuhakikisha hakuna sababu ingine inayopelekea usishike ujauzito ndipo hii iwe sababu ya mwisho. Kuwa na kizazi kilichoinama siyo sababu ya mimba kutokukua vizuri, bali kuwa na ujauzito yaweza kupelekea kizazi kuanguka kwa nyuma.

Kizazi Kuinama na Tendo la Ndoa

Maumivu wakati wa tendo la ndoa ni tatizo linaloondoa furaha kwa wanawake. Bado hakuna sababu ya moja kwa moja inayopelekea maumivu haya kwa wanawake wenye kizazi kilchoinama. Japo baadhi ya nadharia zinasema kwamba maumivu yanaweza kutokana na namna uume unavoingia na kukandamiza mlango wa kizazi, Tishu laini zinazosapoti kizazi zinaweza kutenguliwa na hivo kupelekea maumivu wakati wa tendo. Ni muhimu kwa wapenzi kuzungumza kuhusu staili gani ya kufanya tendo ambayo haimuumizi mwanamke.

Vipimo Kugundua kama Kizazi chako Kimeinama.

Pelvic examination husaidia kugundua kizazi kilichoinama. Daktari ataingiza vidole viwili kwenye uke, kisha mkono mwingine kuweka kwenye tumbo na kusuka taratibu kuelekea kwenye vidole vya ndani ili kuupata mfuko wa mimba, hii itasaidia kujua shape, size na uelekeo wa kizazi.

Wanawake wanaoapata maumivu wakati wa tendo la ndoa na dalili zingine za kizazi kuinama kama nilivoorodhesha pale juu wanatakiwa kumwona daktari haraka. Dallili hizi zinaweza kuashiria pia tatizo lingine baya la kiafya, ndiomaana kuna umuhimu wa kugundua mapema ili uanze kutibu mapema.

Tiba Kupitia Mazoezi

Wakati mwingine daktari wako anaweza kubadili ukaaji wa kizazi bila kufanyiwa upasuaji, kwa maana hiyo utajitaji kufuata utaratibu wa mazoezi ambayo hulenga kukaza misuli inayoshikilia kizazi. Mfano wa mazoezi hayo ni Kegels. Mazoezi mengine yanajumuisha

KNEE CHEST

pelvic exercise

Lala kwenye sakafu (unaweza kutanguliza kipande cha nguo). Mikono ikiwa imeshika kichwa, kunja goti mpaka ikaribie kugusana na kifua, fanya kama picha inaoeleza hapa chini. Tulia katika hali hiyo kwa sekunde 20 mpaka 30 kisha pumzika. Rudia zoezi husika mara 10 mapak 15 kwa kubadilisha miguu

PELVIC CONTRACTIONS

Mazoezi haya yanalenga kuimarisha misuli ya nyonga. Jinsi ya kufanya zoezi hili lala kwenye floor huku mikono yako ikiwa imenyooka kuelekea kwenye miguu. Taratibu nyanyuka eneo la katikati na makalio kuelekea juu kama picha inavoonesha hapa chini. Tulia hivo hivo kwa sekende 30 kisha pumzika, rudia zoezi hili mara 10 mpaka 15 kwa ssoma iku.

KUPANGA JINSIA ZA WATOTO

 

Hatua za Kupanga Jinsia ya Mtoto

Kwa miaka mingi watu wamakuwa wakitafuta njia kama inawezekana kuchagua jinsia ya mtoto kabla mwanamke hajashika ujauzito. Ni kama ilivo kawaida tu pale mwanamke anapojifungua ndugu na jamaa hutaka kujua kama ni mwanamke au mwanaume. Najua unajiuliza mnawezaje wewe na mpenzi wako mkawa na mchango katika kuchagua jinsia ya mtoto. kama hii ni kiu yako ya muda mrefu basi makala hii itaweza kukata kiu yako endelea kusoma

Mbegu za Mwanaume

Kikawaida mwanaume huzalisha aina mbili za mbegu, mbegu ya kike yani (X) na mbegu ya kiume yani (Y), na mwanamke yeye anakuwa na mayai ya kike tu yani X. Ili mtoto awe wa kiume inabidi mbegu Y ya mwanaume ikutane ya yai lenye X ili kufanya (XY) na ili mtoto wa kike afanyike inabidi mbegu ya kike (X) kutoka kwa Mume ikuta na X ya mke kufanya XX. Tafiti za kisayansi zinasema kwamba mbegu ya kiume-Y ni ndogo, dhaifu lakini zenye spidi zaidi ya kuogelea kuliko mbegu ya kike X ambayo ni kubwa, yenye nguvu lakini iko taratibu katika kuogelea. Kutokana na sababu hizi kuna vitu wewe na mwenza wako mnaweza kufanya ili kupelekea mtoto wa kiume au wa kike.

1.Kujua vizuri Mzunguko wa Medhi kwa Mwanamke

Ni muhimu mke na mume kujua vizuri mzunguko unachukua siku ngapi, na ni mzunguko mfupi wa sku 28 ama mrefu wa kuanzia siku 31. Fahamu pia ni siku gani yai linatolewa kwenye mfuko wa mayai ama kwa kifupi siku ya hatari.

Utajuaje hii ndio Siku ya Hatari?

Njia ya kwanza ni kuhesabu mpangilio wako wa hedhi kuanzia siku ya kwanza kupata hedhi kwenye mwezi husika. Tumia kalenga kufatilia siku zako. Angalia mzunguko wako kama unachukua siku 28 basi yai hutolewa siku ya 14.
Kumbuka siyo kila mwanamke anapata yai siku ya 14, wengine huwa na mzunguko mrefu zaidi. Kwa mzunguko mrefu angalia dalili zingine za kutolewa kwa yai kama hizi
Kubadilika kwa ute: ute huwa mzito na mweupe kama eneo jeupe la yai.
Kupanda kwa joto la mwili (Basal body temperature): Joto la mwili huongezeka taratibu baada ya ovulation. Unaweza kupima mabadiliko ya joto la mwili kwa kutumia kipima joto asubuhi baada tu ya kutoka kitandani. Ili kujipa uhakika wa siku ya ovulation fatilia mizunguko mingi ya hedhi upate siku sahihi ambayo yai hutolewa.
Unaweza kutembelea phamacy kupata vifaa ambavyo hupima mkojo kujua mabadiliko ya homoni.
Sasa turudi kwenye mada yetu husika: unapofanya ngono karibu na siku ya yai kutolewa(yani siku ya 14, kunauwezekano mkubwa wa kupata mtoto wa kiume, hii ni kwasababu mbegu za kiume zina spidi sana ya kuogelea kwahivo zinawahi kufika kwenye yai la kike na kulirutubisha.
Kama utashiriki mapenzi siku 3 au zaidi kabla ya yai kutolewa ama ukashiriki tendo siku ile ile ya 14, chansi ya kupata mtoto wa kike ni kubwa kwa sababu mbegu za Y ni dhaifu na zinakufa mapema. Kumbuka mbegu kutoka kwa mwanaume huweza kukaa kwenye tumbo la uzazi kwa siku mpaka 5 zikisubiri yai litolewe ili lirutubishwe.

2.Mazingira ya ndani ya Uke

Mazingira ya ndani ya uke huchangia zaidi katika jinsia ya mtoto. Kama mazingira yana utindikali kwa wingi, chansi ya kupata mtoto wa kike ni kubwa kwani hali hii ya utundikali inaua mbegu dhaifu za kiume na kuziacha mbegu za kike (X). Kwa upande mwingine kama uke una alkali kwa wingi basi chansi ya kupata mtoto wa kiume ni kubwa. Kwahivo kwa kesi hii ili kutengeneza mazingira ya alakali osha uke mpaka ndani kwa maji yenye baking soda kabla ya tendo la ndoa ili kupata mtoto wa kiume. Kwa upande wa pili osha uke kwa maji yenye vinegar ya apple ili kushika mimba ya mtoto wa kike.

3.Staili ya Kufanya Mapenzi

Aina ya mkao wakati mnafanya ngono pamoja na kiasi gani uume umepenya kwenye uke vinachangia katika kuchagua jinsia ya mtoto. Hapa ifaamike kwamba eneo la mwanzo la uke linakuwa na utindikali kwa mwingi ukilinganisha na eneo la ndani la uke ambalo lina alkali kwa wingi.

Uume unaopenya zaidi unazipa mbegu za kiume muda mfupi wa kuogelea kuelekea kwenye yai na kulirutubisha, wakati upande mwingine mbegu zinapotua eneo la mwanzo la uke ambapo pana utidikali kwa wingi inazipa mbegu za kike mazingira mazuri kwani zina nguvu ya kuongelea kwa muda mrefu na katika mazingira ya tindikali.
Tunashauri staili ya mbuzi kagoma (chuma mboga) ili kupata mtoto wa kiume na staili ya kifo cha mende kwa mtoto wa kike.

4.Mwanamke kufika kileleni

Kufika kileleni kwa mwanamke kunaathiri utindikali kwenye uke. Mwanamke anapofika kileleni mwili hutoa kemikali ambazo hupunguza utindikali ukeni na kuongeza alkali kwahivo kuongeza chansi ya kupata mtoto wa kiume. kwa upande mwingine ili kupata mtoto wa kike basi mwanamke asifike kileleni.

5.Wingi wa Mbegu za Kiume

Wingi wa mbegu ni muhimu katika akupata mtoto wa jinsia yoyote. Mbegu kidogo hupelekea mwanamke asishike kabisa mimba. Mwanaume anapokuwa na mbegu nyingi zaidi, chansi ya kupata mtoto wa kiume ni kubwa.

Ushauri zaidi ili kuchagua jinsia ya mtoto

  • Unapojaribu kutafuna mvulana usifanye ngono kwa siku 3 mpaka 4 kabla ya siku ya 14 yaani siku ya hatari. Kupata msichana fanya ngono kila siku kwa siku 3 na pumzika kufanya ngono siku tatu kabla ya siku ya hatari ya 14.
  • Kwa mwanamume avae nguo pana za ndani zisizo za kubana kwa muda wa week moja kabla ya siku ya 14 ambapo atakukutana mwenza wake. Kuvaa nguo pana husaidia mbegu za kiume (Y) kustahimili na kuwa nyingi.
  • Ili kupata msichana mwanamume anashauriwa kuoga maji ya vuguvugu kabla ya kushiriki tendo la ndoa hii ni kupunguza mazingira mazuri kwa mbegu za kiume na hivo kutoa mazingira mazuri kwa mbegu za kike.

Mwisho kabisa

Nashauri kama unajaribu kupata mtoto mvulana, mwanaume atumie kikombe cha kahawa nusu saa kabla ya kufanya ngono.

Kumbuka kama utafatilia vizuri sheria na maelekezo kwenye makala yangu, uhakika wa kupata jinsia ya mtoto unayotaka ni asilimia 70 mpaka 75. Tunashauri pia kufatilia mpangilio wa hedhi kwa ukaribu zaidi kwa muda wa miezi mitatu mpaka minne ili kufanya timing vizuri.

MADHARA YA PUNYETO

  Tiba ya madhara ya upigaji punyeto. Mwanaume mwenye mawazo Kundi kubwa la wanaume wamepungukiwa uwezo wa tendo la ndoa kutokana na kitendo...