Kwanini Kisimi kinawasha na Kuvimba?
Utangulizi kuhusu Kisimi
Kisimi au kinembe ni kiungo kinachoonekana mwanzoni mwa uke kwa juu, kazi ya kiungo hiki ni kuchochea hisia na kumfanywa mwanamke kufikia kilele katika tendo la ndoa. Kisimi kinaweza kuonekana kidogo kwa juu lakini napenda ufahau kwamba kisimi kimejichimbia zaidi kueekea ndani kama mzizi na ni kiungo kikubwa. Tutazungumzia changamoto kadhaa wanazopata wanawake kama kisimi kuvimba, kupanuka, na kuwasha. Endelea kusoma kufahamu zaidi.
Je kuna Size Sahihi ya Kisimi?
Japo hakuna kiwango cha kawaida cha kisimi, lakini najua wafahamu kiwango au size ya kila siku ya kisimi chako. Mara kadhaa kuna baadhi ya hali au shughuli huweza kusababisha kuvimba kwa kisimi kwa muda flani mfano kuongezeka kwa hisia za mapenzi, na kuna sababu zinazoweza kupelekea kuvimba kwa kisimi kwa muda mrefu.
Kuvimba kisimi kwa siku chache
Kuvimba kisimi kwa mda mfupi ni kawaida kama mwanamke ameamshwa kihisia. Hisia za kimapenzi zinapokuwa juu,mzunguko wa damu huongezeka kuelekea kwenye via vya uzazi. Kisimi pamoja na mashavu ya uke huongezeka ukubwa katika hichi kipindi, na kupungua ukishafika kileleni.
Kama mwili wako unasisimuliwa mara kwa mara kimapenzi, na usifike kileleni, basi kisimi kinaweza kuendelea kuwa kimetutumka kwa mda mrefu zaidi.
Vitu vimngine ikiwemo maambukizi vinaweza kuwa chanzo cha kuvimba kwa kisimi pamoja na mashavu ya uke. Mashavu ya uke yanaweza kuvimba kutokana na
Aleji na vifaa au kemikali, nguo, cream au manukato
Maambukizi ya fangasi na bacteria
Kupiga punyeto na kuingiliwa na kitu kwa muda mrefu kwenye uke.
Kuvimba kisimi kwa Zaidi ya wiki
Kama tatizo linafikia wiki moja na zaidi linaweza kuwa limesababishwa na
Matatizo ya homoni
Kuwa na homoni nyingi za kiume (androgens) kama testosterone huweza kupelekea kisimi kuongezeka ukubwa.
- Wanawake wenye polycystic ovarian syndrome (PCOS) na matatizo mengine ya homoni wanapata changamoto hii ya kukua kwa kisimi.
- Vimbe kwenye Mayai (Ovarian Tumors)
- Uvimbe kwenye mifuko ya mayai huanza kuzalisha homoni za kiume kwa wingi na hivo kuepelekea kuongezeka kwa ukubwa wa kisimi.
Lini unatakiwa Kumwona Daktari
kama kisimi au kinembe chako hakirudi katika hali ya kawaida ndani ya siku mja basi unatakiwa kumwona daktari. Unatakiwa pia kumwona daktari kama unapata dalili zingimne kama maumivu na kutokwa na majimaji aidha damu au uchafu. Ni kwa sababu dalili hizi zinaweza kuashiria maambukizi kwenye uke.Hakikisha unamwona daktari unapoona tu dalili zisizo za kawaida. Usisubiri mpaka tatizo liwe kubwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
hauluhusiwi kutoa mauoni kwa lugha ya matusi AU kumkashifu mtu