Alhamisi, 3 Desemba 2020

HEZI SARAMA

 

Mwongozo wa hedhi salama

Hedhi salama ni ipi

Kwa mwanamke kuwa na mzunguko mzuri wa hedhi ni jambo la kujivunia na linaloleta heshima kwako kama mwanamke.
Mzunguko wa hedhi unaweza kutoa picha kamili nini kinaendelea kwenye mwili wa mwanamke, kama mfuko wa mimba unapata mzunguko mzuri wa damu, homoni zako zinbalansi, au kama mayai yanatolewa kwenye ovari. Katika makala yetu ya leo tutaangali hatua za mzunguko wa hedhi, jinsi ya kutumia viashiria ya hedhi ili kujua afya yako na jinsi ya kutumia tiba asili (natural therapies) kama fertility cleansing, tiba za mimea, ama lishe katika kuweka mzunguko wenye afya.

Hedhi ni kitu gani?

Hedhi ni muunganiko wa yai ambalo halikurutubishwa pamoja na damu inayotokana na kumomonyoka kwa tishu laini za ukuta wa mfuko wa mimba (uterus). kitendo hiki hutokea kila mwezi kwa mwanamke.
Jinsi mwili unafofanya kazi mpaka kupatikana kwa hedhi
Kupata hedhi ni kitendo kinachoratibiwa na mzunguko wa homoni . Kwa maelezo mafupi na rahisi ni kwamba inaanza na eneo la ubongo linaloitwa hypothalamus kuzalisha homoni ya gonatrophin (GnRH) ambazo zinachochea tezi ya pituitary kuzalisha homoni ya luteinizing(LH) na Follicle stimulating hormone(FSH), homoni hizi mbili yaani LH na FSH hulenga kuamrisha Ovari kuzalisha homoni za estrogen na progesterone. Ovari napenda kuita ni kiwanda cha kuzalisha na kuhifadhi mayai.
Kwa haraka unaweza kusema ni kitendo rahisi, fikiria hmomoni hizi zinafanya kazi kama vile mfano wa vitabu vilivyopangwa mezani kwa wima vikilaliana, ikitokea kitabu cha mwanzo kimeondolewa kwenye mstari basi vyote vinaanguka.Nii mlolongo mrefu na kama ikitokea mvurugiko wa homoni moja basi mtiririko wote unaharbika na unaanza kukosa hedhi au hedhi kuvurugika, na matatizo mengine mengi ya uzazi ikiwemo uvimbe na ugumba. Zifuatazo ni hatua za mzunguko wa hedhi.

Hatua za Mzunguko wa hedhi

  1. Follicular phase

    Sehemu ya ubongo inayoitwa hypothalamus hutambua kiwango cha estrogen na progesterone ambacho huzalishwa na ovari. Kama kichocheo cha estrogen kikipungua ndani ya mzunguko wa hedhi basi ubongo hutoa GnRH ambayo huamrisha pituitari kuzalisha FSH ambayo inachochea kuanza kukua kwa mayai kuanzia 10 mpaka 20, kati ya haya ni yai moja pekee ambalo hukomaa na kuwa tayari kurutubishwa ndani ya mwezi husika.
    kadiri mayai madogo yanavokuwa huzalisha homoni ye estrogen ambayo kazi yake ni kuimarisha na kuundaa ukuta wa uterus ili kupokea kiumbe baada ya urutubishaji kufanyika.
    Kadiri kiwango cha estrogen kinavyopanda ndivyo mwanamke ataanza kupata ute mzito wa rangi ya maziwa. KUongezeka kwa kiwango cha estrogen huchochea utolewaji wa GnRH kutoka kwenye ubongo ambayo huchochea FSH na LH kwa wingi, homoni hizi mbili huchangia utolewaji wa yai kwenye kikonyo chake kitendo hiki huitwa ovulation. Baada ya ovulationlation kiwango cha FS na LH huanza kupungua taratibu.

  2. Luteal phase
    Kutolewa kwa yai unafuatiwa na hatua hii ya Luteal. kabla ya kuendelea nataka ufahamu baadhi ya misamiati: Kumbuka baada ya yai kutolewa kwenye kikonyo linabaki kovu kama shimo, kovu hili huitwa corpus luteum, kazi yake ni kuendelea kuzalisha progesterone na kiwango kdigo cha estrogen. Ukuta wa juu mwembamba wa uterus ambao humomonyoka tunauita endometrium. Kwahivo baada ya yai kutolewa progesterone inasaidia kuendelea kuurutubisha ukuta(endometrium) ili uweze kupokea kiumbe.
    Endapo hapatawepo na mbegu ya kiume(sperm) kurutubisha yai basi ukuta wa endometrium huanza kubomoka na kutolewa nje kama hedhi.

Jinsi ya Kuhesabu Siku za Mzunguko wa Hedhi

Siku ya kwanza ya mzunguko ni siku ambayo unapata hedhi katika mwezi husika. Siku zote kati kuanzia siku ya kwanza ya hedhi mpaka siku ya ovulation (yai kutolewa) huitwa follicular phase. Kipindi hiki kikawaida huchukua siku 14 lakini hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke.
Luteal phase ni kipindi kati ya ovulation(siku ambapo yai limetolewa) na siku ya kwanza kupata hedhi katika mwezi,ni katika kipindi hiki ambapo yai lililorutubishwa hujishikiza kwenye ukuta wa uterus. Kama kipindi (luteal phase) kitakuwa kifupi sana chini ya siku 12 basi itakuwa ngumu kwa kiumbe kujishikiza kwenye ukuta.

Hedhi ya Kawaida ni ipi

Najua wanawake wengi mtakuwa mnajiuliza ni mzunguko gani wa hedhi ambao ni wa kawaida kwa mwanamke kuwa nao. Ukweli ni kwamba hakuna jibu la mojakwamoja kwamba mzunguko ule ni wa kawaida kutokana na kwamba miili imetofautiana. Lakni taarifa muhimu za kujua kama mzunguko wako ni mzuri ni kujua jumla ya siku za mzunguko wako, kiwango cha maumivu wakati wa hedhi, rangi na kiwango cha bleed yako, taarifa hizi zinaweza kukusaidia kujua ni aina gani ya lishe au tiba asilia utumie ili kurekebisha na kubalansi hedhi yako.

Urefu wa Mzunguko wa Hedhi

Mzunguko wa kawaida unatakiwa kuchukua siku 21 mpaka 35. Baadhi ya wanawake wanaweza kuwa na mzunguko mfupi zaidi au mrefu kuliko huu. Kiwango cha homoni na utolewaji wa yai ndivyo vinatengeneza uwiano wa mzunguko wa hedhi. kama yai halitatolewa itapelekea kuvurugika kwa hedhi na tena kupelekea yai kutotolewa, inakuwa ni kitu endelevu. Kuna vihatarishi vingi vinavyoweza kuvuruga homoni za kike kimojawapo ikiwa ni msongo wa mawazo.

Jinsi ya kutumia Viashiria vya Hedhi ili Kutambua Uwiano wa Homoni Zako.

Hapa chini nimeelezea uhusiano kati ya viashiria hivi na homoni zako. Lengo langu ni kukuonesha namna ya kuusoma mwili na kuusikiliza pale unapoeda nje ya mstari. Mzunguko wa hedhi ni njia muhimu ya kuusoma mwili kuhusu uwezo wa kushika mimba.

  • Kukosa hedhi
    Kukosa hedhi mara moja inaweza isiwe tatizo. Mpangilio wa homoni ni kitu sinsitive sana na kinaweza kuathiriwa tu na msongo wa mawazo, lakini kwa kiasi kikubwa unaweza kujirekebisha wenyewe. Kukosa hedhi pekee siyo kiashiria kwamba hutaweza kushika mimba, manake yawezekana mayai yanatolewa(ovulation) lakini usipate hedhi. Kukosa hedhi kwa zaidi ya miezi 6 huitwa Amenorrhea na inaashiria kuna tatizo ambalo unahitaji kumwona Dactari haraka.
  • Period fupi
    Mzunguko mfupi unaweza kuleta matatizo kwenye uwezo wa kushika mimba. Baadhi ya vihatarishi ambavyo hufupisha mzunguko wako ni kama kukosa ovulation, upungufu wa virutubisho mwilini, uzito mdogo sana, upungufu wa damu .
  • Period ndefu
    Mzunguko mrefu wa hedhi unaweza kuashiria kuvurugika kwa homoni na yai kutotolewa kwa yai kwenye kikonyo chake. Homoni ya progesterone ambayo hutolewa na mwili husaidia kuzuia bleed kuemdelea. Kama estrogen ni nyingi na progesterone ni kidogo bleed inaweza kuendelea kwa siku nyingi zaidi kuliko kawaida
  • Hedhi nzito na nyingi zaidi
    Kupata hedhi nzito na nyingi kupita kiasi husababishwa na ukuta wa uterus kusisimka zaidi kutokana na wingi wa estrogen, inapelekea ukuta kumomonyoka kupita kiasi. Tatizo hili linaweza kurekebishwa kwa kurekebisha lishe yako na kutumia tiba ya mimea kwa ajili ya kurekebisha homoni. Upungufu wa vitamin A na C inaelezwa kuchangia bleed nzito. unaweza kutumia Virutubisho kama Multivitamin.
  • Hedhi kidogo inayoambatana na maumivu makali ya tumbo
    Kama unapata hedhi nyepesi, nyekundu inaweza kuashiria kwamba mzunguko kwenye mfuko wa mimba ni mdogo. Unaweza kupunguza hali hii kwa kufanya masaji kwenye eneo la tumbo ukitumia mafuta ya castor,ama kitambaa kilicholowekwa kwenye maji ya moto.
  • Hedhi ya damu nyekundu inayong’aa
    Kama hedhi yako inakuwa ni damu nyekundu inayong’aa basi hakuna tatizo endelea kufurahia hedhi yako.
  • Hedhi nzito yenye weusi ama brown
    Hii inaonesha kwamba kuna masalia ya damu ya zamani kwa hedhi iliyopita. Kubaki kwa damu husababishwa na flow ya polepole sana na mzunguko mdogo ndani ya mfuko wa mimba. Unaweza kurekebisha tatizo hili kwa kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha, kufanya masaji eneo la tumbo na pia unaweza kujaribu fertility cleansing package yetu.
  • Hedhi yenye damu mpauko na maji zaidi.
    Kama unapata hedhi ya namna hii inaonesha kwamba damu yako kiujumla haina ubora na inakosa virutubishi muhimu. Kula lishe nzuri husaidia unaweza pia kutumia virutubishi vingine kama Multivitamin na Spiriluna kuimarisha damu yako.
  • Kuganda kwa damu ya hedhi
    Kuganda kwa damu ya hedhi inaweza kuwa siyo jambo na kutisha ukilinganisha na kuganda kwa damu kwenye mishipa ya damu. Lakini yatakiwa kuendelea kufatitilia hedhi yako pia. Kama kuganda kwa hedhi yako kunatokea mara chache hasa mwanzoni mwa period, ni mabonge madogo madogo, yenye rangi nyekundu inayong’aa basi ni salama. Lakini kama unapata mabonge mabubwa na inakuwa mfululizo basi yahitaji kumwona Dactari kupata ushauri. Unatakiwa kumwona Dactari haraka kwani kupata Damu nzito yenye mabongemabonge kama unahisi unaweza kuwa na ujauzito yaweza kuashiria kwamba mimba imeharbika.Tumia maji ya kutosha na kufanya masaji eneo la tumbo kwa kutumia mafuta ya nyonyo (castor) ili kupunguza tatizo hili.
  • Kupata bleed kwenye kipindi kisichokuwa na hedhi
    Bleed katikati ya vipindi vya hedhi ni tatizo linasowachanganya sana wanawake. Yaweza kusababishwa na kuvurugika kwa mpangilio wa homoni (rejea maelezo yangu pale juu)Yai kutotolewa kwenye kikonyo chake(ovulation),
    Uvimbe unaotokana na kukua kupita kiasi kwa tishu laini za ukuta wa uterus(endometriosis),Matumizi ya dawa za kupanga uzazi, Mazoezi magumu naLishe duni
  • Kukosa kabisa hedhi(Amenorrhea)
    Inaweza kutatiza pale ambapo unashika ujauzito lakini hupati hedhi kabisa. Kuwa na mzunguko mzuri ni hatua ya kwanza katika kujua kwamba unaweza kushika ujauzito. Kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kuchangia hedhi yako kuvurugika kama msongo wa mawazo, lishe duni, uzito mdogo sana, kutumia vidonge vya kuzuia mimba, kuvurugika kwa homoni, umri kwenda (kukaribia menopause) na matatizo mengine ya kiafya.

Hatua 4 za kufuata ili kuhakikisha kwamba unapata mzunguko mzuri wa hedhi.

  1. Kusawazisha vichocheo/hormones

    Kama nilivokwisha kueleza pale juu kuna mstari mwembamba sana kati ya hedhi kuwa sawa na kuvuruga kwa hedhi, makosa kidogo tu yanaweza kupelekea kuharibu mpangilio wa vichocheo na hivo kuvuruga hedhi yako. Tumia virutubisho mbalimbali kama Soy power, chai ya Pine pollen na Multivitamin kweka sawa vichocheo vyako.

  2. Kuimarisha uwezo wa ini.
    Ini pamoja na kazi zingine hufanya kazi ya kuondoa homoni zilizozidi mwilini. kama kuna kiwango kikubwa cha estrogen ini linaweza kuzidiwa na kuhitaji usaidizi. Hakikisha unatumia tiba nzuri za mimea na virutubishi asili kusafisha ini lako kila mwezi.
  3. Lishe
    Lishe inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuweka hedhi yako sawa. Ni muhimu kutumia virutubisho vya aina nyingi ikiwemo vitamins, madini, mafuta, vidondoa sumu(antioxidants). Vyakula hivi ni muhimu kutumia kwa wingi kwenye mlo wako wa kila siku. Hakikisha unapangilia ili kila siku upate virutubisho hivi vyote kwenye milo yako.Hapa chni nimeelezea vyakula kwa kila aina vya virutubishi . Nimekupa uhuru wa kupangalia kila mlo, siyo lazima kula vyakula hivi vyote kwa mara moja,lakini ni uhimu kupata virutubisho vyote kwa siku. Vyakula vingi vina vitamin na madini mengi uataona maelezo hapa chini.

     

    • madini ya chuma: vyanzo ni mboga za kijani, maini, mayai na mbegu za maboga(unaweza kutumia pia unga wake kutengeneza chai, ama kuchanganya na uji)
    • Vitamin C na B: vyanzo hoho nyekundu, machnungwa, broccoli, cabbage, nyanya na cauliflower.
    • Omega 3: vyanzo vyake samaki, walnuts, na chia seeds
    • Fibers au kambakamba : vyanzo ni mboga za majani kwa wingi na vyakula visivyokobolewa.
    • Madini ya zinc: mbegu za maboga na nyama
    • Vitamin D: kwa kupata mwanga wa jua walau dak 15 mpaka 20 kila siku. asubuhi au jioni
    • Vitamin E: vyanzo vyake ni mafuta ya olive, spinach, parachichi na almonds
    • Folic acid: vyanzo vyake: maini, spinach na maharage.
    • Vyakula vyenye mafuta mazuri; vyanzo ni mafuta ya nazi, olive, parachichi na karanga
  4. Punguza Msongo wa Mawazo
    Stress huleta matoeko hasikwenye hedhi yako kama usipoweza kujifunza namna ya kudhibiti. Stress za kazi, familia, uchumi binafsi na mengine mengi huvuruga mpangilio wa homoni zako. Stress huongeza utolewaji ya homoni ya cortisol ambayo huzuia uzalishaji wa GnRH (rejea maelezo yake pale juu) na kisha kupelekea mayai kutotolewa kwenye kikonyo(ovulation). Stress kwa wanaume hupunguza uzalishaji wa mbegu za kiume na hamu ya tendo la ndoa kwa wote. Mazoezi husaidia kupunguza athari ya msongo wa mawazo.

Muhimu Kwa mwanamke mwenye Changamoto ya Hedhi

Kwa mwanamke mwenye changamoto ya hedhi kuvurugika ama kukosa hedhi kwa muda mrefu, tunashauri atumie mafuta haya ya Rose , yanasaidia kurekebisha homoni. Mafuta haya yalitotengenezwa kitaalamu kwa kuzingatia uasili wake kutatua changamoto za wanawake kama kukosa hedhi, maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi na kukosa hamu ya tendo

rose oil
mafuta ya rose

Angalizo wakati Unatumia Mafuta ya Rose

Kuna tofauti kati ya mafuta ya rose,rose water, mafuta ya rosemary na mafuta ya primrose. Mafuta mengi ya rose yaliyopo mtaani hayana ubora unaotakiwa na ndio maana tumejitahidi kufanya utafiti na kukuletea mafuta yetu asili ya Rose yasiyochakachukuliwa kwa kuendana na thamani ya pesa yako ili

MIMBA YA MAPACHA

 


Jinsi ya kupata Mimba Mapacha

mapacha wanaofanana

Mimba ya Mapacha

Kwa miaka ya hivi karibuni wanawake wamekuwa wakichelewa sanaa kuanza familia ukilinganisha na miaka ya zamani,ambapo wanawake walikuwa wanaolewa wadogo mpaka miaka 15 wanaanza kujifungua.

Kutokana na hili wanawake kuzaa mapacha imekuwa zaidi kuliko zamani, kwasababu chansi ya kuzaa mapacha ni kubwa kwa wanawake wa umri zaidi ya miaka 35 na waliopata ujauzito kwa kutumia dawa zaidi(fertiliy treatment).
kama nawe unataka kuzaa mapacha fahamu kwamba hakuna formula moja kamili ya kufuata lakini kuna baadhi ya njia unaweza kurekebisha ili kuongeza chansi ya kushika mimba ya mapacha. Fuatana nami na mwisho wa makala utaweza kuamua kama ujaribu bahati yako au la…

Mimba ya Mapacha hupatikanaje?

Mimba hutungwa pale mbegu ya kiume inapokutana na yai la mwanamke na kulirutubisha. Kama kwa kipndi ambacho mke na mume wamekutana kuna mayai mawili yametolewa au yai moja liliorutubishwa kugawanyika kuwa mawili basi mwanamke hupata mimba ya mapacha.

Ainza za Mapacha

Mapacha wanaofanana (identical twins): aina hii ya mapacha hufanyika endapo yai moja liliorutubishwa kugawanyika vipande viwili. Mapacha hawa hufanana vinasaba, sura na jinsia pia.

Mapacha wasiofanana(fratenal twins): Aina hii ya mapacha hutokea pakiwa na mayai mawili yaliyokomaa kwenye kizazi wakati wa urutubishaji, na mbegu za kiume kurutubisha mayai yote mawili. Mapacha hawa wanakuwa na jinsia na vinasaba tofauti.

Kwanini mwanamke anajifungua mapacha, nini hutokea?

Mpaka sasa hakuna sababu za moja kwa moja kuonesha ni jinsi gani mpaka mapacha wanafanyika. Japo baadhi ya sababu huweza kuongeza chansi ya kupata mapacha, sababu hizi ni kama

Umri wa Mwanamke

Tafiti zinasema kwamba wanawake wenye umri mkubwa hasa kuanzia miaka 35 wana chansi kubwa ya kupata mapacha wasiofanana. Hii ni kwa sababu ovari za mwanamke huanza kutoa yai zaidi ya moja kila mwezi katika umri huo. sababu ingine ni kwamba wanawake wa umri mkubwa hutoa kichocheo cha FSH(follicle stilumating hormone kwa wingi) ambacho kazi yake ni kuchochea upevushaji wa mayai.

Familia kuwa na Historia ya Kuzaa Mapacha

Kama kwenye familia yako kama mwanamke ama kwenye familia ya mwanaume kuna mapacha basi una uwezekano mkubwa wa kupata mimba ya mapacha pia.

Kuwa kwenye tiba za kuongeza upevushaji wa mayai

Tiba za changamoto za uzazi ni njia maarufu sana kwatika kushika mimba ya mapacha. Vidonge vya tiba hizi huchochea uzalishaji wa mbegu za kiume na mayai ya mwanamke. Kama mayai mengi yakizalishwa kuna uwezekano kwamba yai zaidi ya moja litakuwa tayari kwa urutubishaji kuongezeka na hivo mimba ya mapacha kupatikana.

IVF(invitro fertilization)

IVF ni njia ya maabara ambapo daktari anatoa yai kwenye kizazi na kisha kupandikiza mbegu ya kiume nje ya kizazi kisha kiumbe kupandikizwa kwenye kizazi tena ili kukua. Njia hii ni ghali na wachache huweza kumudu Gharama zake zaweza kufikia sh milioni 24 za kitanzania.

Muhimu pale unapojaribu bahati yako kupata mapacha kupitia huduma yetu.

  • Pumzika kwa muda mrefu kati ya mimba moja na nyingine. Hii itasaidia mayai kutengenezwa kwa wingi na hivo kuongeza uwezekano wa kupata mapacha.
  • Wenza wote mke na mume wanatakiwa kutumia virutibisho, hivyo ni vyema kushirikishana katika hili ili muweze kushirikiana kufanikisha zoezi.
  • Huduma hii siyo ya uhakika kwa 100% hapana, ni jambo la kuongeza uwezekano , kadiri unavozingatia maelekezo yetu na kutumia virutubisho ndivyo unaongeza uwezekeno wa kupata mapacha
  • Kama una changamoto za uzazi inabidi tukupatie tiba kwanza kabla hujaanza hili zoezi.
  • Zoezi hili litawafaa zaidi wanawake wa umri kuanzia miaka 35 na kuendelea

KIZAZI KUINAMA

 

kizazi kuinama (retroveted uterus)

Kizazi kuinama.

Je umewahi kusikia kuhusu kizazi kuinama?, pengine ndugu , rafiki ama mke wako amefanyiwa vipimo na kugundulika kwamba kizazi chaje kimeinama. Leo nitakupa tafsiri nzuri ya kuinama kwa kizazi na jinsi gani inavoathiri afya ya uzazi kwa mwanamke.

Kuinama kwa kizazi kwa majina mengine ya kitaalamu tunaweza kuita tilted uterus,retroflexed uterus, retroveted uterus au backward uterus ni namna mfuko wa mimba unapovutika kuelekea nyuma zaidi ya mlango wa kizazi badala ya kuvutika kuelekea mbele. Ili uweze kunielewa vizuri angalia picha hapa chini. Picha ya kushoto inaonesha kizazi (uterus) cha kawaida na kinaonekana kimepinda kuelekea upande wa mlango wa kizazi. Picha ya kulia ndio inaonesha kizazi kuinama kuelekea nyuma zaidi.

kuinama kwa kizazi

Dalili Anazopata Mwanamke Mwenye Kizazi Kilichoinama

Kumbuka siyo lazima kupata dalili zote kwa pamoja, kama unapata dalili zisizo za kawaida ni vizuri kufika hospitali ili kufanya vipimo ukaanza tiba mapema. Sasa baada ya kuona dalili tuangalie uhusiano kati ya kizazi kuinama na afya ya uzazi.

Nini Kinasababisha Kizazi kuinama?

Mfuko wa mimba ambacho ndio kizazi tunachozungumzia ni sehemu tupu ambayo inajiweka katika eneo la chini ya nyonga za mwanamke. Kazi yake ni kuhifadhi kichanga baada ya urutubishaji kufanyika. Kizazi cha mwanamke kinaweza kuinama kutokana na sababu mbalimbali kama

  • Kulegea kwa misuli ya nyonga: mwanamke akishafikia kukoma hedhi au baada ya kujifungua, misuli inayosapoti tumbo la uzazi hulegea na hivo kupelekea kizazi kuanguka kwa nyuma kama picha pale juu inavooensha.
  • Kupanuka kwa kizazi kutokana na ujauzito, ama vimbe mbalimbali kama fibroids au vimbe ambazo ni saratani (tumor) zinaweza kusababisha kuinama kwa kizazi.
  • Makovu ama msuguano kwenye nyonga
    Mfuko wa mimba ama kizazi kinaweza kupata makovu kutokana na hali mbalimbali mfano , maambukizi kama PID, uvimbe(endometriosis) ama makovu kutokana na upasuaji uliowahi kufanyiwa kwa kipindi cha nyuma. Makovu haya yanaweza kufanya kizazi kuvutika kuelekea nyuma na kuinama.

Kizazi Kuinama na Uwezo wa Kushika Ujauzito.

Kuinama kwa kizazi inaweza kupelekea ugumu wa kushika ujauzito Lakini athari hii siyo ya mojakwamoja, madaktari wanatakiwa kuhakikisha hakuna sababu ingine inayopelekea usishike ujauzito ndipo hii iwe sababu ya mwisho. Kuwa na kizazi kilichoinama siyo sababu ya mimba kutokukua vizuri, bali kuwa na ujauzito yaweza kupelekea kizazi kuanguka kwa nyuma.

Kizazi Kuinama na Tendo la Ndoa

Maumivu wakati wa tendo la ndoa ni tatizo linaloondoa furaha kwa wanawake. Bado hakuna sababu ya moja kwa moja inayopelekea maumivu haya kwa wanawake wenye kizazi kilchoinama. Japo baadhi ya nadharia zinasema kwamba maumivu yanaweza kutokana na namna uume unavoingia na kukandamiza mlango wa kizazi, Tishu laini zinazosapoti kizazi zinaweza kutenguliwa na hivo kupelekea maumivu wakati wa tendo. Ni muhimu kwa wapenzi kuzungumza kuhusu staili gani ya kufanya tendo ambayo haimuumizi mwanamke.

Vipimo Kugundua kama Kizazi chako Kimeinama.

Pelvic examination husaidia kugundua kizazi kilichoinama. Daktari ataingiza vidole viwili kwenye uke, kisha mkono mwingine kuweka kwenye tumbo na kusuka taratibu kuelekea kwenye vidole vya ndani ili kuupata mfuko wa mimba, hii itasaidia kujua shape, size na uelekeo wa kizazi.

Wanawake wanaoapata maumivu wakati wa tendo la ndoa na dalili zingine za kizazi kuinama kama nilivoorodhesha pale juu wanatakiwa kumwona daktari haraka. Dallili hizi zinaweza kuashiria pia tatizo lingine baya la kiafya, ndiomaana kuna umuhimu wa kugundua mapema ili uanze kutibu mapema.

Tiba Kupitia Mazoezi

Wakati mwingine daktari wako anaweza kubadili ukaaji wa kizazi bila kufanyiwa upasuaji, kwa maana hiyo utajitaji kufuata utaratibu wa mazoezi ambayo hulenga kukaza misuli inayoshikilia kizazi. Mfano wa mazoezi hayo ni Kegels. Mazoezi mengine yanajumuisha

KNEE CHEST

pelvic exercise

Lala kwenye sakafu (unaweza kutanguliza kipande cha nguo). Mikono ikiwa imeshika kichwa, kunja goti mpaka ikaribie kugusana na kifua, fanya kama picha inaoeleza hapa chini. Tulia katika hali hiyo kwa sekunde 20 mpaka 30 kisha pumzika. Rudia zoezi husika mara 10 mapak 15 kwa kubadilisha miguu

PELVIC CONTRACTIONS

Mazoezi haya yanalenga kuimarisha misuli ya nyonga. Jinsi ya kufanya zoezi hili lala kwenye floor huku mikono yako ikiwa imenyooka kuelekea kwenye miguu. Taratibu nyanyuka eneo la katikati na makalio kuelekea juu kama picha inavoonesha hapa chini. Tulia hivo hivo kwa sekende 30 kisha pumzika, rudia zoezi hili mara 10 mpaka 15 kwa ssoma iku.

KUPANGA JINSIA ZA WATOTO

 

Hatua za Kupanga Jinsia ya Mtoto

Kwa miaka mingi watu wamakuwa wakitafuta njia kama inawezekana kuchagua jinsia ya mtoto kabla mwanamke hajashika ujauzito. Ni kama ilivo kawaida tu pale mwanamke anapojifungua ndugu na jamaa hutaka kujua kama ni mwanamke au mwanaume. Najua unajiuliza mnawezaje wewe na mpenzi wako mkawa na mchango katika kuchagua jinsia ya mtoto. kama hii ni kiu yako ya muda mrefu basi makala hii itaweza kukata kiu yako endelea kusoma

Mbegu za Mwanaume

Kikawaida mwanaume huzalisha aina mbili za mbegu, mbegu ya kike yani (X) na mbegu ya kiume yani (Y), na mwanamke yeye anakuwa na mayai ya kike tu yani X. Ili mtoto awe wa kiume inabidi mbegu Y ya mwanaume ikutane ya yai lenye X ili kufanya (XY) na ili mtoto wa kike afanyike inabidi mbegu ya kike (X) kutoka kwa Mume ikuta na X ya mke kufanya XX. Tafiti za kisayansi zinasema kwamba mbegu ya kiume-Y ni ndogo, dhaifu lakini zenye spidi zaidi ya kuogelea kuliko mbegu ya kike X ambayo ni kubwa, yenye nguvu lakini iko taratibu katika kuogelea. Kutokana na sababu hizi kuna vitu wewe na mwenza wako mnaweza kufanya ili kupelekea mtoto wa kiume au wa kike.

1.Kujua vizuri Mzunguko wa Medhi kwa Mwanamke

Ni muhimu mke na mume kujua vizuri mzunguko unachukua siku ngapi, na ni mzunguko mfupi wa sku 28 ama mrefu wa kuanzia siku 31. Fahamu pia ni siku gani yai linatolewa kwenye mfuko wa mayai ama kwa kifupi siku ya hatari.

Utajuaje hii ndio Siku ya Hatari?

Njia ya kwanza ni kuhesabu mpangilio wako wa hedhi kuanzia siku ya kwanza kupata hedhi kwenye mwezi husika. Tumia kalenga kufatilia siku zako. Angalia mzunguko wako kama unachukua siku 28 basi yai hutolewa siku ya 14.
Kumbuka siyo kila mwanamke anapata yai siku ya 14, wengine huwa na mzunguko mrefu zaidi. Kwa mzunguko mrefu angalia dalili zingine za kutolewa kwa yai kama hizi
Kubadilika kwa ute: ute huwa mzito na mweupe kama eneo jeupe la yai.
Kupanda kwa joto la mwili (Basal body temperature): Joto la mwili huongezeka taratibu baada ya ovulation. Unaweza kupima mabadiliko ya joto la mwili kwa kutumia kipima joto asubuhi baada tu ya kutoka kitandani. Ili kujipa uhakika wa siku ya ovulation fatilia mizunguko mingi ya hedhi upate siku sahihi ambayo yai hutolewa.
Unaweza kutembelea phamacy kupata vifaa ambavyo hupima mkojo kujua mabadiliko ya homoni.
Sasa turudi kwenye mada yetu husika: unapofanya ngono karibu na siku ya yai kutolewa(yani siku ya 14, kunauwezekano mkubwa wa kupata mtoto wa kiume, hii ni kwasababu mbegu za kiume zina spidi sana ya kuogelea kwahivo zinawahi kufika kwenye yai la kike na kulirutubisha.
Kama utashiriki mapenzi siku 3 au zaidi kabla ya yai kutolewa ama ukashiriki tendo siku ile ile ya 14, chansi ya kupata mtoto wa kike ni kubwa kwa sababu mbegu za Y ni dhaifu na zinakufa mapema. Kumbuka mbegu kutoka kwa mwanaume huweza kukaa kwenye tumbo la uzazi kwa siku mpaka 5 zikisubiri yai litolewe ili lirutubishwe.

2.Mazingira ya ndani ya Uke

Mazingira ya ndani ya uke huchangia zaidi katika jinsia ya mtoto. Kama mazingira yana utindikali kwa wingi, chansi ya kupata mtoto wa kike ni kubwa kwani hali hii ya utundikali inaua mbegu dhaifu za kiume na kuziacha mbegu za kike (X). Kwa upande mwingine kama uke una alkali kwa wingi basi chansi ya kupata mtoto wa kiume ni kubwa. Kwahivo kwa kesi hii ili kutengeneza mazingira ya alakali osha uke mpaka ndani kwa maji yenye baking soda kabla ya tendo la ndoa ili kupata mtoto wa kiume. Kwa upande wa pili osha uke kwa maji yenye vinegar ya apple ili kushika mimba ya mtoto wa kike.

3.Staili ya Kufanya Mapenzi

Aina ya mkao wakati mnafanya ngono pamoja na kiasi gani uume umepenya kwenye uke vinachangia katika kuchagua jinsia ya mtoto. Hapa ifaamike kwamba eneo la mwanzo la uke linakuwa na utindikali kwa mwingi ukilinganisha na eneo la ndani la uke ambalo lina alkali kwa wingi.

Uume unaopenya zaidi unazipa mbegu za kiume muda mfupi wa kuogelea kuelekea kwenye yai na kulirutubisha, wakati upande mwingine mbegu zinapotua eneo la mwanzo la uke ambapo pana utidikali kwa wingi inazipa mbegu za kike mazingira mazuri kwani zina nguvu ya kuongelea kwa muda mrefu na katika mazingira ya tindikali.
Tunashauri staili ya mbuzi kagoma (chuma mboga) ili kupata mtoto wa kiume na staili ya kifo cha mende kwa mtoto wa kike.

4.Mwanamke kufika kileleni

Kufika kileleni kwa mwanamke kunaathiri utindikali kwenye uke. Mwanamke anapofika kileleni mwili hutoa kemikali ambazo hupunguza utindikali ukeni na kuongeza alkali kwahivo kuongeza chansi ya kupata mtoto wa kiume. kwa upande mwingine ili kupata mtoto wa kike basi mwanamke asifike kileleni.

5.Wingi wa Mbegu za Kiume

Wingi wa mbegu ni muhimu katika akupata mtoto wa jinsia yoyote. Mbegu kidogo hupelekea mwanamke asishike kabisa mimba. Mwanaume anapokuwa na mbegu nyingi zaidi, chansi ya kupata mtoto wa kiume ni kubwa.

Ushauri zaidi ili kuchagua jinsia ya mtoto

  • Unapojaribu kutafuna mvulana usifanye ngono kwa siku 3 mpaka 4 kabla ya siku ya 14 yaani siku ya hatari. Kupata msichana fanya ngono kila siku kwa siku 3 na pumzika kufanya ngono siku tatu kabla ya siku ya hatari ya 14.
  • Kwa mwanamume avae nguo pana za ndani zisizo za kubana kwa muda wa week moja kabla ya siku ya 14 ambapo atakukutana mwenza wake. Kuvaa nguo pana husaidia mbegu za kiume (Y) kustahimili na kuwa nyingi.
  • Ili kupata msichana mwanamume anashauriwa kuoga maji ya vuguvugu kabla ya kushiriki tendo la ndoa hii ni kupunguza mazingira mazuri kwa mbegu za kiume na hivo kutoa mazingira mazuri kwa mbegu za kike.

Mwisho kabisa

Nashauri kama unajaribu kupata mtoto mvulana, mwanaume atumie kikombe cha kahawa nusu saa kabla ya kufanya ngono.

Kumbuka kama utafatilia vizuri sheria na maelekezo kwenye makala yangu, uhakika wa kupata jinsia ya mtoto unayotaka ni asilimia 70 mpaka 75. Tunashauri pia kufatilia mpangilio wa hedhi kwa ukaribu zaidi kwa muda wa miezi mitatu mpaka minne ili kufanya timing vizuri.

KUKOSA HAMU

 


Sababu za mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa

changamoto ya hamu yatendo la ndoa kwa wanawake

Nini kinapeleka Wanawake Kukosa hamu ya Tendo la Ndoa?

Nimekuwa Napata kesi nyingi sana kutoka kwa akina mama hasa  wenye umri kuanzia miaka 25 na kuendelea  wakihitaji msaada kwenye ndoa zao kuhusu dawa ya kukosa hamu ya tendo la ndoa baada ya kujifungua au kabla ya kujifungua, maana hawafurahii tendo la ndoa kama vile inavotakiwa. Tatizo linazidi kuongezeka kwa kasi na wengi hawafahamu chanzo cha tatizo hili hivo inakuwa vigumu kulitibu. Leo tutaongelea chanzo cha tatizo na jinsi ya kuepuka na kulitibu ili uendelee kufurahia unyumba.

Zifuatazo ni sababu za Maumivu wakati wa Tendo la ndoa zinazoletekeza Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa  kwa Mwanamke.

  1. Kuvimba kwa kuta za uke kutokana na kushambuliwa na fangasi au bakteria. Kuta hizi huanza kuwa na vijitundu vidogo vidogo na kadiri muda unavyokwenda bila kutibiwa, vitundu hivi huongezeka ukubwa na kuwa kama vidonda na hatimaye kuta za uke kuanza kumomonyoka na hali hii huondoa kabisa hamu ya kushiriki tendo.
  2. Matatizo ya shingo ya kizazi kutokana na maambukizi ya fangasi maeneo hayo. Kutoka kwa mbegu za kiume muda mfupi  au saa kadhaa baada ya tendo ni dalili kuu ya tatizo hili. Pia mwanaume anapogonga shingo hii ya kizazi wakati wa tendo la ndoa mwanamke huwa kama anatoneshwa kidonda. Hali hii ya mbegu kurudi nje husababisha mwanamke kutoshika ujauzito.
  3. Uvimbe kwenye mji wa mimba/mfuko wa uzazi . Uvimbe huu kitaalam hujulikana kwa majina mengi lakini fibrod ni maarufu zaidi. Huanza kama mbegu ndogo ya mchicha na hukua kama boga kubwa. Mwanamke huongezeka ukubwa wa tumbo na baadaye huonekana kama ana mimba kubwa na watu hushangaa kwa nini hajifungui kipindi chote.
  4. Maumivu wakati wa tendo hasa chini ya kitovu huashiria tatizo kwenye mirija ya uzazi. Yawezekana ikawa ni tatizo la mirija ya uzazi kujaa maji machafu kutokana na kuzaliana kwa vimelea sana eneo hilo

Kitu hiki husababisha mirija ya uzazi kuziba kwani maji haya huwa mazito, kitu ambacho husababisha mayai ya uzazi na mbegu za kiume kushindwa kupenya.

Kutoshika mimba (ugumba) kwa mwanamke aliye kwenye ndoa au uhusiano kwa zaidi ya mwaka mmoja na anasikia maumivu ya aina hii ni kiashiria kikubwa cha tatizo hili.

Kumbuka matatizo ya uzazi unayokutana nayo kama maumivu makali kipindi cha hedhi, ugumba, kukosa hamu ya tendo la ndoa baada ya kujifungua ama kabla ya kujifungua , kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa, kuvurugika kwa hedhi, uzito mkubwa na kitambi  siyo kitu ulichoumbiwa, bali ni matokeo ya maisha unayoishi .

Kwa kifupi matatizo yote haya chanzo chake kikubwa ni kuvurugika kwa homoni za kike au hormonal imbalance. Matatizo haya siyo kwamba ni mabadiliko ya vinasaba kutokana na umri, ila ni matokeo ya mpangilio mbovu wa vichocheo ama homoni zako na hasa homoni za uzazi. Hivo utakubaliana nami kwamba wanawake hawajaumbiwa kupata shida hizi zote hata kama umri wako umeenda, unahitaji kuendelea kufurahia tendo la ndoa. Sawazisha mpangilio wako wa homoni na matatizo yote haya utakuwa umeyakimbiza.

Dalili zifuatazo zinaonesha una Mvurugiko wa Homoni.

Hivo unatakiwa kutumia dalili hizi kujifanyia uchambuzi wewe mwenyewe bila hata kufanya vipimo hospitali tayari utagundua kuwa una tatizo kwenye vichocheo ama homoni zako

  1. Uzito kupungua ama kuongezeka bila mpangilio
  2. Tumbo kujaa gesi na kuhisi umeshiba mda mwingi
  3. Maumivu ya kichwa na kujuskia haupo kwenye mood nzuri
  4. Kupata msongo wa mawazo mara kwa mara
  5. Ugumba ama kutoshika mimba kwa kipindi kirefu
  6. Kukosa hamu ya tendo la ndoa ama kupata maumivu makali wakati wat endo la ndoa
  7. Kuhisi mwili umechoka mara kwa mara
  8. Kuota ndevu na nywele kifuani
  9. Kupungua kwa uwezo wa kumbukumbu
  10. Kutokwa jasho jingi usiku na
  11. Ngozi kukakamaa
  12. Kukosa usingizi
  13. Uvimbe kwenye mfuko wa mimba

Baada ya kujifanyia upembuzi juu ya tatizo lako sasa tuangalie nini cha kufanya ili uweze kutibu dalili hizi kuanzia leo ukiwa nyumbani kwako.

Nataka nikwabie mpenzi msomaji na unayefatilia makala hizi kwa makini, kwamba vitu tunavyoweka tumboni vianchangia karibu 80% ya kuvurugika kwa mpangilio wa homoni zako. Unatakiwa kuwa mvumilivu maana kusawazisha homoni ni kitu endelevu na kinachukua kuda kutokana na kwamba unajenga tabia mpya kwenye mwili wako. Hivo hatua ya kwanza katika kupangilia lishe na mlo wako ni

KUONDOA AMA KUFUTA VYAKULA AMBAVYO NI HATARI KWA MWILI WAKO.

Vyakula hivi ni kama sukari, pombe, ngano, na vyakula vilivyosindikwa. Unachotakiwa kufahamu ni kwamba chakula kibovu huletekeza kuvurugika kwa vichocheo ama homoni zako, mfano unapokula sukari kwa wingi ama vyakula vya sukari mwili mwili kupitia kongosho hutoa insulini kwa wingi ili kubadilisha sukari kuwa mafuta yanayohifadhiwa mwilini, kutolewa kwa insulini kwa wingi hupelekea kupungua kwa uzalishaji wa homoni zinazosaidia muimarisha mfumo wa uzazi.

Vyakula vya ngano pia vyenye protin inayoitwa gluten vinaharibu mpangilio wa homoni zako. Kemikali zinazobaki kwenye vyakula baada ya kupuliza madawa ya kuua wadudu kwenye mimea ni kihatarishi kikubwa cha homoni.

Baada ya kuhakikisha umeondoa vyakula hatarishi ambavyo ni chanzo cha kuvurugika kwa homoni zako sasa unahitaji kuongeza vyakula bora ambavyo vitakusaidia kusawazisha homoni zako. Hakikisha unakula zaidi vyakula vya mafuta, vyakula visivyokobolewa.

  1. Tumia virutubisho vya zinc na soy power . Unaweza kufika ofsini kwetu ukapata virutubisho hivi bila kupata adha ya kuagiza nje ya nchi.
  2. Kufanya mazoezi, mazoezi husaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa matatizo kabla na baada ya hedhi. Fanya mzoezi mepesi unayopenda mfano kutembea umbali mrefu, kukimbia nk.
  3. Epuka msongo wa mawazo, tafuta mazoezi rahisi ya kupunguza na kuepuka msongo wa mawazo kama Yoga, meditation.unaweza kusoma pia kwa kubonyeza hapa mnimeelza njia nzuri za kupunguza na kudeal na msongo wa mawazo.
  4. Hakikisha unapata usingizi wa kutosha walau masaa 8 mpaka 9 kila siku.
  5. Na pia punguza ama epuka kwa kiasi kikubwa matumizi ya pombe na vidonge

Tafiti zinasemaje Kuhusu Tiba za Mimea

Zinc

zinc

Kwa wanawake,madini ya zinc yanahusika katika ukuuaji wa yai . Kama mwanamke atakuwa na upungufu wa zinc, yai halitakomaa vizuri na utolewaji wa yai utazuiliwa , na kusababisha ugumba. Kiwango cha zinc cha kutosha kunamwezesha mwanamke kutumia vichocheo vyake vizuri na hivo kuepusha matatizo kama maumivu wakati wa tendo la ndoa, na hokosa hamu ya tendo la ndoa.

Soy power

soy power

vidonge hivi vilivyotengenezwa kiasili kwa kutumia viambata vya mimea ya Radiz Paeoniae Alba Eztractum na Ganoderma husaidia: kuongeza ufanyaji kazi wa mfuko wa mayai , kuzuia Saratani ya matiti, na kuimarisha afya ya uke na tendo la ndoa kwa wanawake waliokoma hedhi.

Dawa zote zinagarimu Sh 145,000/= tu laki 1 na Elfu 45 tu.  Hapa tutakupatia  virutubisho  vya asili viwili vinavyotumika kwa mda wa week 4. Vitakuacha mwili ukiwa safi bila sumu na homoni zako zimesawazishwa. Kisha utafurahia tena tendo la ndoa kama zamani.

Muhimu kuzingatia

Muhudumu wetu atachukua maelezo ya chanzo cha tatizo lako kabla ya kukupatia dawa na virutubisho hivi, na ikibidi anaweza kupendekeza kuongezewa dawa zaidi ya zilizoandikwa kulingana na tatizo lako na hivo gharama kuongezeka.

MAUMIVU YA NYONGA

 

Maumivu ya nyonga.

Watu wengi wamewahi kusumbuliwa na tatizo hili la maumivu ya nyonga kwa kipindi fulani katika maisha yao. Yaweza kuwa ni dalili za matatizo ya hedhi, constipation, kukua kwa tezi dume,na  matatizo ya neva. Kwa watu wachache tatizo linaweza kuwa sugu hadi kupeleka kukwamisha shuguli zao za kimaisha kama kunyanyua mizigo na kutembea vizuri au kufanya tendo la ndoa kwa uzuri.

Asilimia 60 ya watu wanaopata maumivu sugu ya nyonga bado hawajapatiwa ufumbuzi kufahamu nini kinasababisha maumivu haya kitu ambacho kinaleta wasiwasi kwa mgonjwa sababu atashindwa kujua hatima yake. Kwa mgonjwa kufahamu kinachosababisha maumivu haya ni jambo la msingi zaidi ili ujue tiba sahihi ya kukufaa.

Maumivu ya nyonga ni nini?

Kwa ujumla hakuna njia moja inayoweza kuelezea maumivu haya, ni maumivu yanayotokea sehemu katikati ya tumbo na eneo la hips , kwa baadhi ya watu maumivu yanaweza kuanzia kwenye eneo la chini ya mgongo na kusambaa hadi kwenye eneo la nyonga. Kwa upande wa mwanamke maumivu yanaweza kutokana na shida kwenye uzazi sababu mfumo wa uzazi wa mwanamke upo kwenye nyonga. Maumivu haya ya nyonga yanaweza kumpata mwanamke, mwanaume na hata watoto pia.

Dalili za maumivu ya nyonga

Maumivu ya nyonga siyo ugonjwa bali ni dalili ya uwepo wa tatizo la kiafya. Maumivu haya yanaweza kuwa ya muda mfupi au ya muda mrefu na hutokea kweye nyonga na chini ya tumbo.

Dalili za maumivu  ya nyonga hutofautiana kwa wagonjwa, wengine hupata maumivu mepesi na wengine hupata maumivu makali. Kwa baadhi ya watu maumivu huweza kuwa makali hadi kupelekea kukwamisha shughuli za kimaisha kama mazoezi, kutembea na tendo la ndoa. Kwa ujumla maumivu ya nyonga huambatana na matatizo mengine kama kushindwa kufanya tendo la ndoa vizuri.

Nini kinasababisha maumivu ya nyonga?

Kuna sababu nyingi zinazopelekea maumivu ya nyonga kwa wanawake na wanaume. Inaweza kuwa ni maambukizi, ama athari kwenye viungo vya ndani kama kibofu cha mkojo, utumbo mpana, kwa wanawake yaweza kuwa ni shida kwenye uzazi. Hapa chini ni maelezo sababu kuu zinazopelekea maumivu ya nyonga.

  • Constipation: kukosa choo ama kupata choo kigumu kwa muda mrefu husababisha maumivu ya nyonga kutokana na presha na kujaa gesi kwa tumbo. Constipation yaweza kusababishwa na lishe mbaya, msongo wa mawazo, matatizo ya homoni, upungufu wa madini ya magnesium, kupungua kwa bacteria wazuri tumboni na kutoshugulisha mwili. Kwa kutumia package yetu ya digestive care unaweza kupona tatizo lako la constipation na kuimarisha afya ya tumbo. bonyeza hapa kuanza huduma ya virutubisho asili.
  • Matatizo ya kibofu cha mkojo: kibofu kinapopata hitilafu hupelekea kuvimba kwa tishu zake na kusababisha maumivu kwenye eneo la nyonga. Ugonjwa wa kibofu uitwao interstitial cystitis, ambao huletekeza dalili za UTI ni moja ya matatizo yanayosababisha maumivu ya nyonga.
  • Matatizo ya figo: matatizo kama maambukizi kwenye figo au mawe kwenye figo husababisha maumivu ya nyonga. Tatizo la mawe kwenye figo husababisha maumivu ya chini ya mgongo ambayo husambaa mpaka kwenye eneo la nyonga.
  • Hernia: hernia hutokana na kutofunga kwa eneo la chini ya tumbo na kupelekea kukua kwa tishu kukua kuelekea eneo la uzazi. Hernia husababisha maumivu makali ya nyonga.

Maumivu ya nyonga kwa wanawake

Maumivu ya nyonga kwa wanawake yanaweza na shida kwenye uzazi. Matatizo haya yanaweza kutokea kwenye viungo kama uke, shingo ya kizazi, mirija ya uzazi, mifuko ya mayai au mfuko wa mimba. Inawezekana pia kupata maumivu kutokana na sababu zaidi ya moja, sababu hizi zinaweza kuwa

  • Endometriosis : endometriosisi ni kitendo cha kukua kwa ukuta wa ndani(endometrium) wa mfuko wa mimba kuelekea nje ya mfuko wa mimba. Pale tishu zinapokua na kuwa nene husababisha dalili kama maumivu ya nyonga, maumivu kpindi cha hedhi, tumbo kujaa gesi na maumivu ya chini ya mgongo.
  • Fibroidsfibroids ni uvimbe usio saratani unaotokea ndani ya kuta za mfuko wa mimba. Tafiti zinasema kwamba karibu asilimia 40 mapaka 80 ya wanawake hupata shida ya fibroids katika uzazi kwenye maisha yao.
  • PIDpid ni maambukizi kwenye njia ya uzazi ambayo kwa kiasi kikubwa husababishwa na magonjw aya ngono kama chlamydia au gonorrhea. Dalili kubwa ni maumivu ya nyonga, maumivu wa wa tendo ndoa, maumivu wakati wa kukojoa, na kutokwa na uchafu ukeni kusiko kawaida.
  • Ovarian cysts: ovarian cysts ni mkusanyiko kwa vimbe ndogo ndogo zilizojaa maji kwenye mifuko ya mayai ya mwanamke. Kwa wanawake wengi vimbe hizi hazileti shida na huweza kupotea baada ya muda. Lakini kwa baadhi ya wanawake vimbe zinapokuwa kubwa huleta maumivu ya nyonga na kuvurugika kwa hedhi.
  • Kutoa mimba: dalili kubwa zinazotokea baada ya kutoa mimba ni kama kutokwa na uchafu ukeni usio kawiada, maumivu ya chini ya tumbo, maumivu ya nyonga, kuharisha na wakati mwingine kuzirahi kutokana na kutokwa na damu nyingi.
  • Maumivu kipindi cha hedhi: baadhi ya wanawake hupata maumivu ya nyonga wakati wa hedhi, mumivu haya huitwa dysmenorrhea kwa kitaalamu. Maumivu kipindi cha hedhi ni kutokana na kutanuka kwa misuli ya mfuko wa mimba.

Maumivu ya nyonga kwa wanaume

Ukiacha wanawake, wanaume pia hupata tatizo hili la maumivu ya nyonga, hasa wenye tatizo la tezi dume.. kuvimba kwa tezi dume ama maambukizi kwenye tezi dume husababisha maumivu ya nyonga, eneo la haja kubwa, kwenye tumbo la chini na pia maumivu kwenye kibofu. Dalili zingine zinazoonesha kuna shida kwenye tezi dume ni kupata maumivu wakati wa kukojoa ama kupata mkojo kidogo sana . unapoona dalili hizi wahi hospitali mapema ili kupata vipimo na tiba haraka.

ANGALIZO

Kuna sababu nyingi zinazopelekea maumivu ya nyonga na baadhi ya sababu hizi huashiria magonjwa hatari. Weka mihadi na dactari wako ufanye vipimo ili kujua chanzo cha tatizo. Kumbuka maumivu ya nyonga ni dalili na siyo ugonjwa kwahiyo ni lazima kujua ni ugonjwa gani unapelekea maumivu yako ya nyonga. Hivo basi kama unapata maumivu yasiyokwisha pamoja na kutokwa na uchafu ukeni kwa wanawake onana na dactari haraka hasa pale ukiwa mjamzito, maana inaweza kuwa ni dalili ya kutoka kwa mimba.

BARIDI YABISI

 

Ugonjwa wa Baridi Yabisi

Ugonjwa wa Baridi Yabisi (Arthritis)

Baridi yabisi ni moja ya magonjwa kwenye kundi la (autoimmune diseases) magonjwa yanayotokana na kinga ya mwili kushambulia tishu za mwili na kupekelea tishu hizi kututumka na kuvimba. Tatizo hili huathiri maeneo ya maungo na kuletekeza maumivu makali yasiyokwisha, kuvimba kwa joint na kusababisha ugumu kukunja viungo. Tatizo linaweza kuwa kubwa pale mpambano kwenye joint (inflammation) unapokuwa mkubwa na baadae maumivu hupungua.

Kwa mgonjwa mwenye baridi yabisi ni muhimu kurekebisha lishe na mtindo wa maisha kama ambavyo nitaelekeza hapa chini ili kupunguza makali ya ugonjwa. Ugonjwa wa baridi yabisi kama usipochukuliwa hatua za haraka kuudhibiti unaweza kusababisha matatizo makubwa kama kuharibika kwa maungio, neva na athari kwenye mishipa ya damu.

Baridi yabisi husababishwa na muunganiko wa sababu ikiwemo lishe, vinasaba, mtindo wa maisha, vichocheo pamoja na kinga ya mwili.Tafiti zinasema kwamba kwa mgonjwa anayeanza tiba mapema hupata nafuu zaidi na kuepuka madhara ya baridi yabisi. Pamoja na dawa za hospitali wataalamu wa tiba asili tunashauri mgonjwa azingatie zaidi lishe na mazoezi ili kupunguza maumivu.

Dalili za Mgonjwa Mwenye Baridi Yabisi.

Dalili za Baridi yabisi hutokana na kupotea kwa utando mweupe uliopo mwishoni mwa mfupa (cartilage) ambao hupunguza msuguano kati ya mfupa na mafua, kuvimba kwa tishu zinazozunguka jointi na kukaza kwa joint. Kwa mgonjwa mwenye baridi yabisi ute uliopo kati ya mfupa na mfupa hupungua na kufanya mifupa kusagana. Dalili kuu za mgonjwa mwenye baridi yabisi ni

  • Maumivu ya joint-Kuvimba kwa tishu zinazozunguka maungio ya mifupa husababisha maumivu makali kwa mgonjwa. Jointi zinazoathirika zaidi ni kwenye mikono, enka, vidole vya miguuni na kwenye magoti.
  • Ngozi ya joints kuwa nyekundu, laini na inayochoma kama vile imeungua moto.
  • Maumivu na kushindwa kusonga mbele baada ya kuamka asubuhi, hali hii huchukua dakika 30 na baaade mgonjwa anaweza kuendelea kutembea.
  • Mwili kufa ganzi na maumivu ya misuli
  • Kupata ugumu kwenye kutembea, kushika kitu, kufanya mazoezi na kupanda ngazi.
  • Kwa baadhi ya wagonjwa hupoteza hamu ya kula na kupata homa za muda mfupi.

Madhara gani ya Muda Mrefu Anaweza Kupata Mtu Mwenye Baridi Yabisi.

Kwa baadhi ya wagonjwa wenye baridi yabisi hupata madhara ya kiafya ya muda mrefu mwilini. Tafiti zimebaini matatizo haya huzaliwa na uwepo wa arthritis.

  • Kuongezeka kwa hatari ya kupata magonjwa ya moyo na kiharusi.
  • Maumivu ya kifua, pumzi kukata na kushindwa kupumua kutokana na athari kwenye mapafu.
  • Maumivu ya kichwa yasiyoisha.
  • Matatizo ya figo na kujikusanya kwa maji mwilini
  • Maumivu na kudhoofika kwa mifupa
  • Kuishiwa damu na kupata ganzi
  • Kuota vinyama vidogo vidogo kuzunguka eneo la maungio ambavyo huongeza ukali wa maumivu

Nini Kinasababisha Uugue Baridi Yabisi

Kama nilivoeleza mwanzo Ugonjwa huu ni moja ya kundi la magonjwa ya autoimmune kumanisha kwamba ugonjwa unaletekezwa na mazingira ambayo husababisha kinga yako ya mwili ishambulie kimakosa tishu zinazozunguka maungio ya mifupa.

Swali la msingi ni kwanini kinga ya mwili ishambulie tishu kimakosa? Mpambano kwenye tishu inaweza kuletekezwa na vihatarishi vifuatavyo

  • Kuzorota kwa afya ya mfumo wa chakula
    Lishe mbaya na vyakula vinavyoleta alegi (vyakula vinavyoletekeza mpambano kama vyakula vilivyosndikwa, sukari na vyakula vilivyokaushwa kwa mafuta)
  • Uzito mkubwa na kitambi hasa kwa watu chini ya umri wa miaka 55
    Mazingira yenye sumu ambayo yanaathiri mwili na kuvuruga mpangilio wa homoni, ndomana tunashauri utumie Detox Care Package yetu kutoa sumu kwanza kabla hujaanza tina nyingine.
  • Kushuka kwa utendaji wa kinga ya mwili kutokana na athari za kiafya na
  • Uvutaji wa sigara

Tiba Asili na Jinsi ya Kukabiliana na Tatizo la Baridi Yabisi.

Kwa kutumia virutubisho ukiwa nyumbani.

Mara nyingi madactari wanapogundua una baridi yabisi, watakwandikia vidonge ambavyo ni antiinfammatory na pain killers kwa ajili ya kupunguza mpambano na maumivu kwa muda mfupi. Tatizo la tiba hii ni ya muda mfupi na mgonjwa hurejea katika hali ya mateso akishamaliza kuvitumia, ndiomaana nashauri kulenga chanzo cha tatizo lako na kutumia njia asili kutibu uginjwa wako.Zifuatazo ni hatua salama unazoweza kuchukua ukiwa nyumbani kwako ili upunguze makali ya ugonjwa na kutibu.

  1. Hatua ya kwanza: Tumia Lishe inayosaidia kupunguza kuvimba na kututumka kwa tishu (Anti-inflammatory Diet)
    Wataalamu wa lishe wanashauri matumizi lishe sahihi katika kupunguza kuvimba kwa tishu kutokana na kushambuliwa na kinga ya mwili. Lishe hii inajumuisha vyakula vyenye mafuta mazuri kama mafuta ya kupikia ya nazi,mizeituni, mboga za majani, supu ya mifupa, vyakula vyenye omega 3 kwa wingi kama walanut (lozi) na samaki wa kina kirefu. Ni muhimu pia kuepuka vyakula vinavyoongeza kuvimba kwa tishu za kwenye maungio, vyakula vya ngano, sukari, vyakula vilivyokaushwa kwa mafuta,  na vyakula vyote vilivyosindikwa.
  2. Hatua ya pili: Kufanya mazoezi mara kwa mara:
    Najua unapata maumivu makali kwenye maungio kutokana na ugonjwa wa baridi yabisi, lakini ni muhimu kushugulisha mwili wako ili kupunguza athari ya tatizo. Ndiomaana unapolala ukaamuka asubuhi unapata ugumu kutembea na kuendelea, hakikisha unafanya mazoezi mepesi kila siku wakati huo unazingatia sheria zingine nitakazofafanua.
  3. Hatua ya tatu: Punguza msongo wa mawazo na Hakikisha unapata usingizi wa kutosha
    Kupata usingizi wa kutosha kila siku kuanzia masaa 8 na kupunguza msongo wa mawazo inasaidia joint kujitibu vizuri. Msongo wa mawazo unafanya tatizo kuwa baya zaidi na kukuongezea dalili zingine mbaya kama maumivu ya misuli, kushuka kwa kinga, kushambuliwa na magonjwa, na uzito kuongezeka kupita kiasi.
  4. Hatua ya 4: Tumia njia za asili ili kupunguza maumivu ya jointi, Njia hizi ni kama
    • Kufanya masaji kwenye eneo lililoathirika kwa kutumia mafuta ya eucalyptus.
    • Weka kipande cha barafu kwenye eneo ya maungio yya mifupa

Tiba Kupitia Mafuta ya Eucalyptus na Lavender

Mafuta haya yamekuwa yakitumika kwa zaidi ya miaka 2000 katika kutibu changamoto za misuli na viungo vya mwili. Ni mafuta asili yasiyo na kemikali. Huhitaji tena kuagiza nje ya nchi, tayari tumefanya utafiti na kukuleta mafuta yasiyochakachuliwa ili upate matokeo chanya haraka.

Matumizi: chovya kiasi kidogo cha mafuta na usugue sehemu yenye maumivu walau mara mbili kwa siku. Matokeo utayapata ndani ya siku moja ukianza kutumia. Endelea kutumia mafuta kwa week 2 zaidi kila siku.

AHSANTE KWA KUTUFATILIA WA SAMBAZIE NAWENGINE WAJE KUJIFUNZA 

MADHARA YA PUNYETO

  Tiba ya madhara ya upigaji punyeto. Mwanaume mwenye mawazo Kundi kubwa la wanaume wamepungukiwa uwezo wa tendo la ndoa kutokana na kitendo...