Chanzo Cha Goita Ni Nini?
Chanzo kikubwa cha goita katika sehemu nyingi za dunia ni ukosefu wa madini ya iodine katika chakula. Katika maeneo ambayo madini ya iodine huongezwa kwenye chumvi inayotumika, goita huwa zinatokana na uzidifu au upungufu katika uzalishwaji wa homani ya thyroid au vivimbe vinavyojijenga kwenye tezi ya thyroid.
Tiba hutegemea ukubwa wa goita, dalili ambazo zimejitokeza na chanzo halis cha goita hiyo. Goita ndogo ambazo hazionekani na ambazo hazileti usumbufu hazihitaji tiba.
Dalili Za Goita
Si goita zote ambazo huonyesha dalili. Pale mabapo dalili zitaonekana, zinaweza kuwa:
1. Uvimbe unaooneka eneo inapoanzia shingo
2. Kusikia kubanwa kooni
3. Kukohoa
4. Sauti kukwaruza
5. Shida kumeza
6. Shida kupumua
Chanzo Cha Goita
Tezi yako ya thyroid hutengeneza aina kuu mbili za homoni – thyroxine (T-4) na triiodothyronine (T-3). Homoni hizi mbili huzunguka katika mfumo wa damu na husaidia katika shughuli za kimetaboliki – kujenga na kuvunjavunja kemikali katika mwili. Husimamia namna mwili unavyotumia mafuta na wanga, husaidia kuweka sawa joto la mwili, kurekebisha mapigo ya moyo, na kusimamia uzalishwaji wa protini.
Tezi ya thyroid hutengeneza pia calcitonin – homoni inayosaidia kuweka sawa kiwango cha calcium ndani ya damu.
Tezo za pituitary na hypothalamus husimamia kasi ya utengenezwaji na utolewaji wa homoni hizi.
Mlolongo wa mambo huanza pale hypothalamus – eneo lililo chini ya ubongo linalofanya kazi kama thermostat ya mfumo wako mzima – inapotoa ishara kwa pituitary kutengeneza homoni iitwayo thyroid stimulating hormone (TSH). Tezi ya pitutary ambayo nayo ipo kwenye eneo la chini ya ubongo, itatoa kiasi fulani cha TSH, kulingana na kiasi gani cha thyroxine na T-3 vipo ndani ya damu. Tezi yako ya thyroid, nayo, itarekebisha uzalishaji wa homoni kulingana na kiasi cha TSH kilichotolewa na tezi ya pituitary.
Kuwa na goita hakuamaanishi kuwa tezi yako ya thyroid haifanyi kazi vizuri. Hata wakati imevimba, tezi yako inaweza kuwa inatoa kiasi cha homoni kinachotakiwa. Inaweza kuwa, pamoja na hayo, ikawa inatengeneza homoni za thyroxine ne T-3 kwa kiwango cha juu zaidi au cha chini.
Kuna vipengele vinavyoweza kusababisha tezi ya thyroid kuvimba. Sababu zinazojitokezamara nyingi zaidi ni:
. Upungufu wa iodine.
. Graves’ disease
. Hashimoto’s disease.
. Multinodular goiter.
. Solitary thyroid nodules.
. Thyroid cancer.
. Ujauzito.
. Kuvimba.
Tiba ya Goita
Tiba ya goita inategemea ukubwa wa goita, dalili zinazojionyesha, na chanzo halisi cha goita hiyo. Dakatari anaweza kupendekeza yafuatayo:
. Uangalizi. Kama goita yako ni ndogo na haileti madhara, na tezi yako ya thyroid inafanya kaz ivizuri, daktari anaweza kuchukua uamuzi wa kuiacha na kuitazamia.
. Madawa. Kama tezi yako inafanya kazi chini ya kiwango (hypothyroidism), unaweza kuongezewa homoni kwa kutumia levothyroxine (Levoxyl, Synthroid, Tirosint) ambavyo pia vitapunguza utolewaji wa TSH kutoka tezi ya pituitary, hatua ambayo mara nyingi hupunguza ukubwa wa goita.
Pale panapokuwa na vivimbe kwenye tezi ya thyroid, daktari anaweza kukuandikia spirin au dawa ya corticosteroid kuuondoa uvimbe.
Goita zinazotokana na utendaji wa kupitiliza wa tezi (hyperthyroidism), utahitaji dawa za kupunguza viwango vya homoni.
. Upasuaji. Kuondoa sehemu au tezi yote ya thyroid (total or partial thyroidectomy) ni uamuzi endapo goita ni kubwa sana na inaleta usumbufu au kusababisha shida katika kupumua au kumeza.
Upasuaji ni tiba pia kwa saratani ya tezi ya thyroid.
Unaweza kuandikiwa kutumia levothyroxine baada ya upasuaji, kulingana na kiasi cha tezi ya thyroid kilichoondolewa.
. Radioactive iodine. Wakati mwingine, radioctive iodine hutumika kutibu tezi ya thyroid inayozidisha utoaji wa homoni. Radioactive iodine hunywewa na huifikia tezi ya thyroid kupitia mzunguko wa damu, na kuua seli za thyroid. Matokeo ni kupunguza ukubwa wa goita, lakini pia huweza kusababisha utendaji mdogo wa tezi hiyo.
SAMBAZA KWENYE MITANDAO YA KIAMI NA WENGINE WAJIFUNZE TOA MAONIYAKO KWA NI MUHIMU SANA KWETU baruth5.blogspot.com/
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
hauluhusiwi kutoa mauoni kwa lugha ya matusi AU kumkashifu mtu