Fangasi Sugu
Fangasi sugu (Candidiasis)
Kwenye makala hii utajifunza dalili za fangasi, nini kinachosababisha upate fangasi sugu na aina ya lishe unayotakiwa kutumia ili kutibu fangasi.
Candida ni nini?
Candida ni aina ya fangasi ambao wanapatikaa kwenye mdomo, uke, tumbo la chakula na wenye ngozi. Katika hali ya kawaida ya mwili fangasi hawa hawaleti madhara na pia husaidia shuguli za mwili. Pale inaopotokea kinga ya mwili kushuka fangasi hawa huanza kukua kupita kiasi na kuleta madhara.
Fangasi wa candida wanaweza kukua na kusambaa mpaka kwenye mfumo wa damu, kwenye ubungo na kusababisha tatizo kuwa sugu endapo halitatibiwa mapema.
Hali ya tindikali kwenye mwili inapokuwa kubwa huchangia pia kukua zaidi kwa fangasi hawa wa candida na kusababisha dalili mbaya na aleji kwa vyakula. Mgonjwa anaweza kupata aleji ya vyakula kama mayai, maziwa na vyakula vya ngano.
Nini Kinapelekea Upate Fangasi Sugu
Pamoja na matumizi makubwa ya lishe yenye sukari na wanga iliyokobolewa hapa chini ni sababu zingine zinazopelekea upate fangasi sugu
1.Matumizi ya Muda Mrefu ya Antibiotics
Antibiotics ni dawa muhimu zinazotumika kuua bakteria wabaya kwenye mwili wako, japo lengo linaweza kuwa ni zuri lakini shida ni kwamba antibiotics haziui bakteria wabaya pekee bali hata wale wazuri ambao ni kinga dhidi ya fangasi. Matumizi ya muda mrefu hupelekea mwili kuwa sugu na kutosikia uwepo wa antibiotics na hivo kufanya mazingira mazuri ya fangasi kumea.
2.Vidonge vya Kupanga Uzazi
Wanawake wanaotumia vidonge vya kupanga uzazi wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kupata fangasi sugu. Hii ni kutokana na kuvurugika kwa mazingira ya kawaida ya homoni.
3.Dawa za asthma
Wagonjwa wanaotumia dawa za pumu kwa kutumia kifaa cha mdomono(inhaler) wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kupata fangasi sugu mdomoni. Hakikisha unafata maelekezo ya kusafisha mdomo kila baada ya kutumia kifaa hichi. Kama umeanza kupata dalili za fangasi mdomoni unaweza kusafisha mdomo wako kwa kutumia mafuta ya nazi. Tumia pia kirutubisho hichi cha cha Cordiceps kuimarisha kinga na kupunguza dalili mbaya za pumu.
4.Dawa za Kutibu Saratani
Tafiti zinaonesha kwamba kwa wagonjwa wa saratani, fangasi inaweza kusambaa haraka zaidi na kuleta madhara. Hii ni kutokana na tiba ya mionzi(radiotherapy) na dawa(chemotherapy) anayotumia mgonjwa wa saratani, tiba hizi hupunguza kinga ya mwili na kupelekea fangasi wa candida kusambaa. Wagonjwa wa saratani wanashauriwa kutumia Vidonge vya ginseng na ganoderma ili kuzuia kukua kwa seli za saratani na kuimarisha kinga.
5.Kisukari (Diabetes)
Sukari na mwili wenye tindikali inachochea ukuaji wa fangasi. Wagonjwa wa kisukari wapo kwenye hatari zaidi ya kupata fangasi sugu kutokana na mwili kushindwa kurekebisha kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu.
Tunashauri wagonjwa wa sukari kutumia majani ya chai ya basalm na vidonge vya chitosan ili kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu na kuimarisha afya zao.
6.Kuzorota kwa Kinga ya Mwili
Watu wenye kinga dhaifu ni rahisi zaidi kuugua fangasi sugu. Makundi ya watu hawa ni pamoja na watoto, wazeee, na wenye ugonjwa wa ukimwi. Kwa wagonjwa wa ukimwi tunawashauri kutumia kirutubisho hiki cha A power ili kuimarisha kinga zao na hivo kupunguza maambukizi ya fangasi ya mara kwa mara.
Dalili za Fangasi Sugu
1.Mwili kukosa nguvu mara kwa mara.
Kama unapata uchovu kupita kiasi na mwili kukosa nguvu mara kwa mara unaweza kuwa na tatioz linalojulikana kitaalamu kama chronic fatigue syndrome. Ugonjwa huu huambatana na uchovu wa zaidi ya miezi 6 na dalili zingine kama maumivu ya kichwa, jointi na kupoteza kumbukumbu.
Madaktari wengi wanaamini kwamba kukua kupita kiasi kw afangasi wa candida ni chanzo kikubwa cha ugonjwa huu wa chronic fatigue syndrome.
2.Maambukizi mara kwa mara Ukeni na UTI sugu
Kama unapata maambukizi ya UTI na fangasi ukeni kila mara, basi kwa kiasi kikubwa fangasi wa candida wanaweza kuwa ndio chanzo cha tatizo lako. Kumbuka kwamba fangasi wanaweza kuambukizwa kupitia ngono hivo ni muhimu kufanya ngono salama na wanawake kuepuka kuvaa nguo zilizobana na kuacha kuoga maji ya moto ukiwa na fangasi.
4.Utando Mweupe Kwenye Ulimi
Fangasi hawa wanaweza kuambukizwa kwa kufanya ngono kupitia mdomo na romans pia. Kwa watoto wanaweza kuambukizana kwa kushea vitu vya kuchezea. Wagonjwa wa pumu pia wanaweza kupata fangasi mdomoni kwa kutumia dawa ya kuvuta(inhaler) kwa amuda mrefu.
5.Maambukizi Kwenye eneo la Ndani la Tishu za pua(Sinus Infections)
Fangasi wa candida wanaweza kuleta athari kwenye tushu laini za ndani ya pua na kusababisha mgonjwa kukohoa mara kwa mara, mafua na aleji. Kama unapata kuuugua huku mara kwa mara na mafua yasiyoisha ni muhimu kucheki kama una maambukuzi ya fangasi wa candida.
5.Changamoto za Mfumo wa Chakula(Intestinal Distress)
Tumbo kujaa gesi mara kw amara, kujamba, kukosa choo na kupata choo kigumu ama kuharisha ni kiashiria kwamba kuna ukuaji wa fangasi kupita kiasi kwenye mfumo wa chakula. Fangasi wanaanza kukua kupita kiasi hupelekea kupungua kwa bakteria wazuri ambao husaidia kwenye kuchakata chakula na kinga. Mgonjwa anapokua chakula kinachelewa au kutosagwa vizuri na hivo kutengeneza gesi tumboni na hali ya kuharisha.
6.Ubongo kutofanya kazi vizuri(brain fog)
Pamoja na uchovu wa mara kwa mara na mwili kukosa nguvu, fangasi hawa wa candida wanaweza kupelekea kushindwa ufanya maamuzi vizuri na kupoteza kumbukumbu.
7.Maambukizi Kwenye Ngozi na Kucha
Fangasi kwenye kucha na kwenye ngozi ni matokeo kwamba vimelea hawa wa candida wamekua kupita kiasi kwenye mwili.
Ushauri kwa Mgonjwa Wa Fangasi Sugu
- Mafuta ya nazi yana uwezo mkubwa katika kupambana na fangasi kutokana na uwepo wa viambata hai vya lauric acid na caprylic acid. Tumia kwa kupakaa eneo lililoathirika na pia kupikia kwenye chakula. Hakikisha unapata mafuta asili yasiochanganywa na kemikali.
- Tumia kirutubisho asili cha Garlic oil capsule chenye vidonge 60, tumia dozi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
hauluhusiwi kutoa mauoni kwa lugha ya matusi AU kumkashifu mtu