Jumapili, 25 Oktoba 2020

FANGASI UKENI

 

Ni ipi dawa asili ya kutibu fangasi ukeni (vaginal candidiasis)

Mamilioni ya watu kwa sasa wanapambana na kiumbe mwenye seli moja asiyeonekana, ambaye ni fangasi anayeitwa Candida.  Maambukizi ya fangasi sehemu za siri imekua ni tatizo kubwa sana Duniani 75%ya wanawake wote Duniani wanasumbuliwa na tatizo hili na wanatafuta dawa ya fangasi ukeni kila siku. Maambukizi haya ya fangasi katika sehemu za siri za mwanamke yakisababishwa kwa kiasi kikubwa  na fangasi aina ya Csndida Albicans, na maambukizi haya pia hujulikana kama Yeast infection/Yeast thrush.

Fangasi Ukeni Husababishwa Na Nini?, Je Kuna tiba ya Fangasi?           

Kikawaida vimelea hawa wa Candida Albicans hupatikana katika midomo, mpira wa kupitishia chakula (Pharynx), kibofu cha mkojo, uume au katika uke na kwenye ngozi pia. Bacteria hawa huishi katika sehemu hizo bila kuleta  madhara, isipokua pale mazingira ya eneo husika, yanapobadilika, mfano mabadiliko katika hali ya PH tutambue PH ya mwanamke ndani ya uke ni 4.0-4.5 au uwiano wake na vimelea (microorganisms) wengine, hivyo huharibiwa kutokana na sababu mbalimbali pia kupungua kwa Kinga ya mwili kutokana na magonjwa mbalmbali huletekeza kukua kwa Candida, ndio maana wagonjwa wenye maradhi ya ukimwi na saratani ama wanaopata matibabu ya mionzi huwa kwenye hatari kubwa ya kuumwa fangasi ya Candida.

Candida pia hupatikana kwenye mdomo, tumbo, kwenye kwapa,  hivo pale inapotokea fangasi hawa wa Candida kuanza kukua kupita kiasi bila kudhibitiwa kitendo hicho huitwa Candidiasis ama Yeast infection,matokeo yake ni mfululizo wa maambukizi na kuumwa kwa mwili .

Bahati mbaya ni kwamba taarifa nyingi za mtandaoni zimekuwa zikipotosha pasipo kueleza kwa ufasaha juu ya tatizo hili na hivo kufanya uelewaji wa tatizo kuwa mgumu. Hivo kama unasumbuliwa na tatizo hili na unapenda kujifunza na unahitaji kujua kuhusu dawa asili ya fangasi sugu basi endelea kusoma makala hii kwa umakini mpaka mwisho.

Ni muhimu kuelewa kwamba kukua kupita kiasi kwa Candida siyo kwasababu Candida wanapatikana kwenye eneo husika, hapana na ndio maana tatizo linakuwa gumu kutibika kutokanana na kwamba dawa nyingi huua Candida wote na kuua bacteria wazuri na hivo kuharibu msawazo wa mwili. Kumbuka uwepo wa Candida ni muhimu kwa ufanisi wa mwili.

Fangasi Ukeni (Vaginal Candidiasis)

Maambukizi ya fangasi ukeni yanaweza isiwe ugonjwa hatari pale unapanza, lakini, huleta usumbufu na harufu kali na hivo mgonjwa kukosa amani. Baadhi ya mambo yanayoongeza hatari ya kupata maambukizi ya fangasi ukeni ni ujauzito, kuumwa kisukari, kushuka kwa kinga ya mwili kutokana na kuugua magonjwa mbalimbali na pia matumizi yaliyokithiri ya dawa hasa zile za kuua bacteria/antibiotics. Wanawake wapo katika hatari kubwa zaidi ya kuugua fangasi za sehemu za siri ukilinganisha na wanaume, lakini pia hata wanaume huambukizwa tatizo hili.

Je Upo Kwenye Makundi ya Tabia hizi Hatarishi Kupata Fangasi?

Kwa wanawake kuna baadhi ya tabia hatarishi zinazoongeza chansi ya kupata maambukizi ya fangasi wa Candidiasis.

  • Ngono mara kwa mara na watu tofauti tofauti bila kinga
  • Kufanya ngono kupitia mdomo
  • Matumizi makubwa ya mipira wakati wa ngono mfano Condoms
  • Matumizi makubwa ya tissue za kujisitiri/ huitwa pantliners
Mambo mengine hatarishi yanayopelekea kukua kwa fangasi wa Candida kwa wote mwanaume na mwanamke;
  • Matumizi yaliyokithiri ya antibiotics
  • Kuugua kwa mda mrefu ugonjwa wa Kisukari.
  • Kiwango kikubwa cha homoni za uzazi.
  • Vinasaba na
  • Uvutaji wa sigara

Maambukizi ya fangasi ukeni yamegawanyika katika sehemu KUU mbili nazo ni ÷
(1)MAAMBUKIZI YASIYO MAKALI (UNCOMPLICATED THRUSH)
~katika aina hii mgonjwa hupatwa na maambukizi Mara moja hadi nne kwa mwaka pia Dalili zake huwa si za kuogopesha na maambukizi haya husababishwa na fangasi aina ya CANDIDA ALBICANS
(2)MAAMBUKIZI MAKALI (COMPLICATED THRUSH)
Katika kundi hili mgonjwa hupatwa na maambukizi Zaidi ya Mara nne au Zaidi kwa mwaka pia Dalili zake huwa ni za kuogopesha kama maambukizi yatakua yametokea kipindi cha UJAUZITO, ugonjwa wa VVU, ugonjwa wa sukari nk

VIHATARISHI VINGINE VINAVYOPELEKEA KUPATA FANGASI  (CANDIDIASIS)
  • Mabadiliko ya mfumo wa homoni mwilini ambazo husababisha mabadiliko katika sehemu za siri
  • Magonjwa ya saratani ya tezi koo la Chakula (thyroid cancer)
  • Wanawake wenye umri wa miaka 20-30 wapo katika hatari ya kupata maambukizi haya wakati wale ambao wamekoma hedhi (menopause) na wale ambao hawajaanza kupata hedhi hawako katika hatari kutokana na mazingira na vitu wanavyotumia.
  • Matumizi ya vidonge vya majira
  • Msongo wa mawazo uliokithiri ;
  • Kujamiana kwa njia ya kawaida Mara tu baada ya kujamiiana kupitia haja kubwa (anal sex)
  • Matumizi ya vilainishi wakati wa kujamiiana husababisha maambukizi pia
  • Kuwa na historia ya kupata matibabu ya homoni (hormonal replacement therapy)
  • kuwa na utapiamlo (malnutrition), kuvaa nguo za ndani zisizo kauka vizuri na kuvaa mavazi yanayoleta sana joto sehemu za siri.

DALILI ZA UGONJWA WA FANGASI UKENI 

  • Kuwashwa sehemu za siri
  • Kuhisi maumivu makali wakati wa kujamiiana
  • Kuhisi kuwaka moto sehemu za siri Mara baada ya kutoka kufanya tendo la ndoa au kutoka kukojoa (burning sensation .
  • Kupata vidonda ukeni (soreness) .
  • Kuvimba na kuwa mwekundu katika mdomo wa nje wa uke (labia minora
  • Kupata maumivu wakati wa kukojoa na
  • Kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au kijivu unaoweza kuwa mwepesi au mzito au majimaji
    NOTE :Dalili na viashiria hivi huwa mbaya Zaidi mwanamke anapokua mwezini
MATIBABU NA JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA HUU WA FANGASI UKENI na dawa asili ya fangasi sehemu za siri..

Matibabu ya ugonjwa huu wa fangasi hupatikana hospitali  na kutolewa kupitia vipimo vya uchunguzi na majibu yalivyotoka. Pamoja na hayo matibabu ya ugonjwa huu hospital sio ya uhakika kwasababu dawa za hospital hazitibu chanzo cha tatizo hivyo ndio maana tatzo hili huwa Linajirudia baada ya muda fulani, pia ugonjwa huu unaweza kujikinga nao kwa kuepuka mambo mbalimbali na kuzingatia kanuni ya afya na usafi.

  • Vaa nguo za ndani ambazo hazibani na zilizotengenezwa kwa pamba au Hariri
  • Epuka kufanya mapenzi na mpenzi wako mwenye maambukizi haya mpaka pale atakapotibwa na kupona kabisa.
  • Kula mlo wenye virutubsho muhimu.
  • Epuka kuoga maji ya moto sana (Hot baths) tumia maji ya uvuguvugu
  • Osha sehemu zako za siri kwa kutumia maji Safi na jikaushe kwa kutumia taulo au kitambaa Safi.
  • Epuka mavazi yote ya kubana ukeni.
  • Kunywa maziwa aina ya mtindi yenye live culture Mara kwa Mara yatakusaidia kuepusha maambukizi ya fangasi ukeni.
  • Epuka matumizi ya vifaa vya kupanga uzazi na vifaa vya kufanyia mapenzi (sex toys, diaphragm cervical caps) husababisha maambukizi ya fangasi ukeni
  • Epuka kutumia sabuni za kemikali/dawa kuoshea ukeni.

Muhimu kwa Wagonjwa wa Fangasi ukeni

Kwa mwanamke mwenye changamoto ya fangasu sugu , tunashauri atumie Uterus cleansing pill kusafisha kizazi ili kuondoa maambukizi haya. Uterus cleansing pill (UCP) ni vidonge 3 vilivyotengenezwa kitaalamu kwa kuzingatia uasili wa dawa kutatua changamoto za wanawake kama kupata harufu mbaya ukeni, maambukizi ya fangasi na bacteria, PID na kuziba kwa mirija ya uzazi.

vidonge vya kusafisha kizazi
uterus cleansing pills

Vidonge vya Uterus cleansing vinatumika kwa siku 15. Kidonge kimoja kinawekwa ukeni na kutolewa baada ya siku 3, kisha unapumzika siku 2,unaweka tena kidonge kingine. Havitumiki kwa wajawazito, bikira na kipindi cha hedhi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

hauluhusiwi kutoa mauoni kwa lugha ya matusi AU kumkashifu mtu

MADHARA YA PUNYETO

  Tiba ya madhara ya upigaji punyeto. Mwanaume mwenye mawazo Kundi kubwa la wanaume wamepungukiwa uwezo wa tendo la ndoa kutokana na kitendo...