Kwanini Unapata UTI sugu?
Maambukizi kwenye njia ya mkojo (UTI)ni maambukizi yanayoshika nafasi ya pili kuupata mwili mara nyingi zaidi. Maambukizi haya hufanya mtu kukosa raha na kwa baadhi ya watu hasa wanawake ni tatizo la kiafya linalojirudiarudia mara nyingi. Kwa bahati mbaya ni kwamba tiba iliyozoeleka kwa UTI ni kutumia antibiotics ambapo bacteria wanaosababisha UTI wanaoitwa E.coli wameanza kuwa sugu dhidi ya hizi antibiotics na hivo kupelekea wagonjwa wengie kupata UTI sugu. Kwa upande mwingine kuna tiba asili ambazo unaweza kujitibu ukiwa nyumbani na ukapona ugonjwa huu pasipo kutumia vidonge vya antibiotics
UTI sugu Ni Kitu Gani?
UTI ni kifupi cha maneno urinary tract infection yaani maambukizi kwenye njia ya mkojo. UTI ni mkusanyiko wa maambukizi eidha ya fangasi, virusi au bacteria ambayo yanatokewa kwenye njia ya mkojo ya mwanamke na mwanaume. Tunaposema njia ya mkojo tunaongelea figo zote mbili, mirija inayotoa mkojo kutoka kwenye figo hadi kwenye kibofu cha mkojo huitwa ureter, kibofu chenyewe,na mrija wa kutoa mkjo nje kutoka kwenye kibofu. Kazi ya figo ni kuchuja maji yaliyopokwenye damu na kutoa maji yaliyozidi, na takamwili. Baada yah apo mkojo huifadhiwa kwenye kibofu na baadae kutolewa nje kupitia mrija wa urethra ambayo una misuli ya sphincter iliyopo kwenye uke na uume.
Bacteria wanaopatikana kwenye kinyesi ndo kwa kiasi kikubwa husababisha UTI. Bacteria hawa wanapoingia kwenye njia ya mkojo mwili kwa kutumia kinga yake huweza kuwadhibiti, lakini inaposhindikana ndipo bacteria hawa husababisha madhara. Kitendo cha kukukojoa mara kwa mara husaidia kusafisha bacteria waliojishikiza kwenye njia ya mkojo, na pia tezi dume hutoa majimaji kwa mwanaume ambayo huzuia ukuaji wa bacteria wabaya. Japo kuna kinga kubwa ya mwili dhidi ya UTI lakini bado kuna hatari ya kuugua ugonjwa huu ndio maana tunatakiwa kuwa makini zaidi.
Dalili Za UTI
Zifuatazo ni dalili za moja kwa moja kwa watu wazima
- Kupata maumivu makali wakati wa kukojoa
- Kujiskia hali ya kuchomachoma kwenye kibofu wakati wa kukojoa
- Kujiskia kukojoa mara kwa mara, na kupata mkojo mdogo sana
- Maumivu ya misuli
- Maumivu ya tumbo la chini
- Mkojo kuwa mwekundu au wa pink( dalili ya damu kwenye mkojo)
- Mkojo unaonuka zaidi
- Maumivu ya nyonga kwa wanawake
- Wakati mwingine kushindwa kujizuia mkojo kutoka
Aina Za Maambukizi Kwenye Njia Ya Mkojo (UTIs)
Kuna aina nyingi za maambukizi katika njia ya mkojo. Maambukizi yanayotokea kwenye mirija ya urethra huitwa Urethritis, na dalili zake ni kama maumivu ya mgongo wa chini, homa kali, mwili kutetemeka na kutapika, urethritis yaweza kusababishwa na Bacteria wa E. coli na Virusi pia wa herpes simplex.
Kama maambukizi yametokea kwenye kibofu basi huitwa cystitis. Dalili za athari kwenye kibofu ni kama maumivu ya nyonga, mkojo wa mara kwa mara unaoambatana na maumivu makali na mkojo wenye damu.
Bacteria pia wanaweza kusafiiri mpaka kwenye figo na kuathiri figo, aina hii ya maambukizi tunaita pyelonephritis. Dalili za kuwa figo zimepata athari ni maumivu wakati wa kukojoa hii ni kutokana na uwepo wa mawe ya figo ambayo hukwama kwenye mirija ya kutolea mkojo.
Sababu Na Mazingira Hatarishi Yanayopelekea Upate UTI Sugu
Maambukizi kwenye njia ya mkojo hutokea pale bacteria wanapoingia kwenye njia ya mkojo, kujishikiza na kuanza kukua mpaka kuleta athari. Ukifahamu kinachosababisha UTI basi ni rahisi kwako kuepuka na hutasumbuka tena kupata UTI sugu kila mara, yafuatayo ni mazingira hatarishi yanayoongeza uwezekano wa kupata maambukizi haya.
Wanawake
Wanawake wapo hatarini zaidi kupata maambukizi kwenye njia ya mkojo kutokana na kwamba njia yao ya mkojo kuelekea kwenye kibofu ni fupi kwahiyo bacteria wanaweza kusafiri haraka zaidi na kuleta athari kwenye kibofu, sababu ingine ni kwamba njia ya kutolea mkojo kwa mwanamke kwenye uke ipo karibu zaidi na mahali pa haja kubwa penye bacteria waletao maambukizi.
Kufanya Ngono
Utafiti uliofanyika katika chuo kikuu cha Washington kitengo cha tiba unaonesha kwamba moja ya kihatarishi kikubwa kwa wanawake wa umri wadogo kupata UTI ni kujihusisha na ngono. Ngono huweza kuhamisha bacteria kutoka kwenye mdomo wa uke mpaka kwenye mirija ya urethra. Ndio maana inashauriwa kwa mwanamke kupata mkojo na kukojoa mara baadaya ya kufanya ngono ili kuflash bacteria wabaya.
Njia Za Kupanga Uzazi
Baadhi ya njia za kupanga uzazi huweza kuongeza hatari ya kupata mambukizi kwenye njia ya mkojo. Matumizi ya condoms huweza kufanya Ngozi itutumke na hivo kuwa rahisi kwa bacteria kushambulia tishu laini za uume au uke.
Wajawazito.
Maambukizi kwenye njia ya mkojo ni tatizo kubwa kwa wanawake. Watafiti wanaamini kwamba mabadiliko ya vichocheo vya uzazi wakati wa ujauzito hupelekea kuhama kwa njia ya mkojo na hivo kuongeza hatari ya kupata maambukizi ya UTI. Kutokana na kuhama kwa njia ya mkojo hupelekea bacteria kusafiri mpaka kwenye figo na kuleta athari kirahisi. Ndio maana kuna umuhimu kwa wajawazito kufanyiwa vipimo vya mkojo mara kwa mara.
Wanawake Waliokoma Hedhi
Grupu lingine ambalo lipo kwenye hatari zaidi ya kupata UTI ni wale waliokoma hedhi. Utafiti unasema kwamba upungufu wa kichocheo cha estrogen kwa wanawake hawa huchangia ukuaji wa bacteria. Na changamoto kubwa kwa wahanga wa UTI ni kwamba huwa inajirudia rudia. Kadiri unavougua zaidi basi ndipo hatari ya kuugua tena huongezeka. Japo wanaume wapo kwenye hatari ndogo ya kupata UTI, hatari ya kuugua tena inaongezekana kwa wale waliowahi kuugua maana vimelea hujificha kwenye tezi dume.
Tiba Asili Za Kutibu Na UTI Sugu Na Kujikinga Kuugua UTI Mara Kwa Mara
- Hakikisha unakunywa maji ya kutosha: maji haya husaidia kuflash bacteria wabaya kabla hawajaleta athari
- Neda haja ndogo mara kwa mara. Unapopata haja ya kukojoa basi usisubiri neda katoe mkojo mara moja, na pia ni muhimu kukojoa baada ya kufanya ngono ili kuwasafisha wale bacteria walioingia kwenye njia ya mkojo.
- Kwa mwanamke jipanguse kuanzia mbele kwenda nyuma hasahasa baada ya kwenda haja kubwa, hii ni kuhakikisha bacteria hawaingii kwenye njia ya mkojo .
- Vaa nguo kubwa zisizobana: uvaaji wa nguo pana zisizobana hasa za ndani husaidia hewa kuzunguka na kukausha njia ya mkojo na hivo kuzuia kukua na kumea kwa bacteria.
- Tumia virutubisho kwa ajili ya kuimarisha kinga ya mwili na kuongeza. Watafiti wanasema uwepo wa bacteria wazuri (normal flora na kinga imara ya mwili husaidia kuepusha maambukizi ya UTI. unaweza kutembelea stoo yetu kwa kubonyeza hapa ili uanze huduma ya virutubisho
- Kitunguu saumu: kitunguu saumu kina tabia ya kuua bacteria, matumizi ya kitunguu saumu mara kwa mara ni moja ya tiba asili ambayo unaweza kutumia ukiwa nyumbani japo unatakiwa kutumia kiwango kikubwa mpaka kupona, ndio maana tunashauri utumie virutubisho ambavyo tayari vimetengenezwa katika mfumo wa vidonge maaana vina kiwango kikubwa cha dawa ndani yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
hauluhusiwi kutoa mauoni kwa lugha ya matusi AU kumkashifu mtu