Jumapili, 18 Oktoba 2020

 DALILI ZINAZO KUTAMBULISHA KUWA UNA UGOJWA AU HATALI YA KUPATA UGOJWA WA BAWASIRI 

Dalili za bawasiri hutofautiana. Wakati mwingine hakuna dalili zinazojitokeza na mtu anaweza asijue kuwa ana bawasiri.

Dalili ya kawaida kabisa ni kutokwa na damu wakati ukienda kujisaidia haja kubwa. Damu huonekana iliyo mbichi, nyekundu, juu ya toilet tissue, kwenye sahani ya choo au ikiwa imekizunguka kinyesi.

Bawasiri huweza kuchomoza na kuning’inia nje. Mara nyingi unaweza kuzisukuma na vidole zikarudi ndani baada ya kujisaidia. Lakini bawasiri zilizofikia hali mbaya huning’inia moja kwa moja nje na huweza kuzisukuma ndani.

Bawasiri ndogo za ndani kwa kawaida hazina maumivu. Bawasiri kubwa huweza kutoa majimaji, kuwa na maumivu, na kuwasha. Majimaji yatokayo yanaweza kuchubua eneo linalolizunguka tundu la haja kubwa. Unaweza kuwa na hisia za kuwa na haja kubwa au kuwa hujamaliza vizuri haja zako ukiwa unatoka msalani.

Matokea mabaya ya bawasiri zinazoning’inia ni kuwa zinaweza zikajifinyanga na kusababisha damu kushindwa kupita kuelekea kwenye bawasiri hizo, hali ambayo inaweza kuleta maumivu makali sana. Mara chache inaweza ikatokea kuwa damu ikaganda ndani ya bawasiri (thrombosis) hizo, hali ambayo huleta maumivu makali pia.

 

Tiba Ya Bawasiri

 

Kukwepa Kufunga Choo Na Kutumia Nguvu Wakati Wa Haja Kubwa

Jaribu kuweka kinyesi kuwa laini na usitumie nguvu wakati wa kujisaidia haja kubwa. Unaweza kufanya yafuatayo:

Tumia nyuzinyuzi kwa wingi kama matunda, mboga za majani, nafaka n.k.

 

intestine cleansing tea

Intestine Cleansing Tea: Bofya Juu Ya Picha Kwa maelezo

 

 

Tumia vinywaji kwa wingi. Watu wazima yafaa kunywa angalau lita 2 kwa siku (glasi 6-8). Utatoa maji mengi kama mkojo lakini mengine yataingia tumboni na kulainisha kinyesi. Vinywaji vya karibu aina zote vinafaa, lakini pombe husababisha mwili kupoteza maji kwa hiyo siyo nzuri sana. Matumizi ya kahawa kwa wingi nayo siyo mazuri.

 

bawasiri chanzo chake

 

Nyuzinyuzi Za Kiada. Kama chakula chenye nyuzi nyuzi kwa wingi hakisaidii, unaweza kutumia nyuzinyuzi za kiada kama ispaghula, methylcellulose, bran au sterculia. Unaweza kuvinunua hivi kutoka kwenye maduka ya madawa. Methylcellulose inasaidia pia kulainisha kinyesi na kukifanya kiweze kupita kirahisi.

 

Meal Cellulose Tablet

Meal Cellulose kutoka Green World. Bonyeza juu ya picha kusoma maelezo.

 

Acha kutumia dawa za kupunguza maumivu zenye codeine. Kama co-codamol, kwa sababu nuwa ni chanzo cha kufunga choo. Dawa za kawaida kama paracetamol husaidia.

Kujisaidia Inapotakiwa. Nenda chooni mara moja baada ya kusikia haja kubwa. Watu wengine hujibana na kufikiria kwenda kujisaidia baadaye. Tabia hii hufanya ukubwa na ugumu wa kinyesi kuongezeka na kuleta shida wakati wa kukitoa. Usijikamue kwa nguvu wakati wa haja kubwa. Usitumie muda mwingi chooni, kwani inaweza kusababisha ujikamue. (Kwa mfano, usisome wakati ukiwa chooni).

Hatua hizi zitakusaidia usitokwe na damu au kukosa raha. Inaweza kuwa ni tiba kwa bawasiri ndogo na zisizochomoza na kuning’inia nje (Grade 1). Bawasiri ndogo za garde 1 huweza kuondoka zenyewe baada ya muda.

 

Mafuta Na Cream

Aina mbalimbali za bidhaa za mafuta na cream zinaweza kutumika. Bidhaa hizi si kwa ajili ya kuponya bawasiri bali kupunguza hali ya kujisikia vibaya na miwasho. Bawasiri za mimba huondoka zenyewe baada ya kujifungua.

 

Tiba Ya Banding

Banding ni tiba inayotolewa kwa bawasiri za grade 2 au 3. Inaweza pia kutumika kutibu bawasiri za grade 1 pale ambapo hatua za hapo juu zitakuwa hazikusaidia.

Daktari wa upasuaji hutumia vifaa maalumu kuzivuta bawasiri na kufunga rubber band kwenye shina la bawasiri hizo. Kwa kufanya hivyo, damu haitafika kwenye bawasiri hizo, ambapo zitakufa baada ya siku chache. Kidonda hupona chenyewe na kuacha kovu.

Banding ya bawasiri za ndani mara nyingi haileti maumivu kwa sababu vishina vya bawasiri hizo huota kwenye eneo ambalo halina mishipa ya neva. Bawasiri hadi tatu huweza kutibiwa kwa njia hii kwa wakati mmoja.

Asilimia 20 ya bawasiri zilizotibiwa kwa njia hii huweza kuota upya siku za baadaye. Lakini tiba ya banding huweza kurudiwa tena. Uwezekano wa bawasiri kukurudia utakuwa mdogo kama tahadhari zitachukuliwa, ikiwa ni pamoja na kuacha kujikamua wakati wa haja kubwa.

Watu wachache huweza kupata madhara zaidi baada ya tiba hii, kama kutokwa na damu, matatizo ya kukojoa, maambukizi ya wadudu au kuota uvimbe kwenye eneo lililokuwa na bawasiri.

nakuomba ndugu jama na malafiki SAMBAZA au SHEA iliwanao sumbuliwa waweze kupata na kujua wachukue hatua zipi 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

hauluhusiwi kutoa mauoni kwa lugha ya matusi AU kumkashifu mtu

MADHARA YA PUNYETO

  Tiba ya madhara ya upigaji punyeto. Mwanaume mwenye mawazo Kundi kubwa la wanaume wamepungukiwa uwezo wa tendo la ndoa kutokana na kitendo...